Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko LHRC yaitaka serikali kuboresha sheria zinazokandamiza wanawake
Habari Mchanganyiko

LHRC yaitaka serikali kuboresha sheria zinazokandamiza wanawake

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

IKIWA leo tarehe 8 Machi 2018 Tanzania na dunia nzima inaadhimisha siku ya wanawake duniani, serikali imeendelea kusisitizwa kuboresha sera na sheria zinazohusu wanawake ili kuimarisha ustawi wao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga akiwa nchini Marekani.

Henga ameitaka serikali kuendelea kufanya maboresho baadhi ya vifungu vyenye mapungufu vinavyokandamiza haki za wanawake katika sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya mirathi.

“Ni vizuri tukawa na sera na sheria nzuri dhidi ya wanawake, sheria hizo zitasaidia wanawake kuwa na ustawi. Sheria za mirathi na zinazohusu ukatili wa wanawake zifanyiwe marekebisho,” amesema Henga.

Aidha, Henga ameitaka jamii kubadilisha mtazamo na fikra hasi dhidi ya wanawake ikiwa pamoja na kuondoa mfumo dume, badala yake iheshimu na kutimiza haki za wanawake.

“Jamii tubadilishe mtazamo, na fikra kwa kuwa na mtazamo chanya kwa wanawake sababu wako wengi idadi yao ni zaidi ya asilimia 50. Hivyo tukibadilisha mtizamo juu yao tutaleta amani, maendelea na mafanikio kwa jamii,” amesema Henga.

Tarehe 8 Machi kila mwaka ni siku ambayo dunia huadhimisha siku ya wanawake, ambapo huitumia siku hiyo kuangalia changamoto na mafanikio ya wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

error: Content is protected !!