May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

LHRC: Uhuru wa kujieleza umeminywa

Spread the love

 

RIPOTI ya Haki za Binadamu Tanzania Bara (LHRC), kwa mwaka 2020 imeeleza, uhuru wa kujieleza umeendelea kuminywa kutokana na utungaji, marekebisho na utekelezaji wa sheria zinazominya uhuru kujieleza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika ripoti hiyo iliyozinduliwa leo tarehe 9 Aprili 2021 na Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imeeleza, mabadikilo ya sheria na utungaji wa sheria mpya umeathiri kwa kiasi kikubwa uhuru wa kujieleza.

Pia amesema, kumekuwa na matukio na ukatili ambao mara nyingi ukielekezwa kwa wanawake, na kwamba, haki zilizovunjwa zaidi kwa mwaka 2020, zinajumuisha haki ya kuishi ambapo matukio ya kujichukulia sheria mkononi yapatayo 443 yameripotiwa.

Pia ukatili dhidi ya wanawake umeendelea kuongezeka kwa mwaka 2020, na kufikia matukio 26,544 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo yalikuwa matukio 23,683.

Amesema, ripoti hiyo imeangazia matukio ya ubakaji na ukatili wa kimwili kwa watoto na ambayo kitakwimu yameonekana kuongezeka.

“Matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto yaliripotiwa zaidi kutoka mikoa ya Pwani, Simiyu na Tabora. Ndoa za utotoni matukio yapatayo 35 yameripotiwa ambapo mikoa iliyoongoza ni pamoja na Katavi, Shinyana na Arusha,” amesema Henga.

“Kuheshimu haki za binadamu ni muhimu sana kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla,” ameeleza Hanga.

Ripoti hiyo imeeleza kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika matukio mabaya wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ikilinganishwa na mwaka 2015.

“Kutokana na juhudi za wadau, asasi za kiraia na jeshi la polisi, matukio ya namna hiyo hayakuwepo sana. Tunashukuru kwa juhudu hizo,” imeelezwa ripoti hiyo huku ikisistiza kuwepo kwa hofu kubwa wakati wa uchaguzi mkuu huo.

Ripoti hiyo imeeleza, ajali za barabarani zimepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2019. Mwaka 2016 matukio ya ajali yaliripotiwa 10,297 ambapo mwaka 2019 yaliripotiwa 2,924.

“Ajali zimepungua kwa kiwango kwa silimia 56 kutoka mwaka 2016 hadi 2019,” imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.
Henga ameiomba serikali kuhakikisha inaimarisha haki ya haki za binadamu nchini na kuleta mabadiliko makubwa.

error: Content is protected !!