WAKATI jirani zetu nchi ya Kenya wakimaliza uchaguzi wao , Ubora wa Katiba yao umetajwa kuwa sababu ya kutokuwa na machafuko licha ya changamoto zilizojitokeza. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea)
Hayo yamesemwa leo tarehe 19 Agosti 2022 na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu nchini (LHRC) Anna Henga, wakati akizundua mpango maalum kuelekea siku ya Demokrasia Duniani tarehe 15 Septemba 2022.
Amesema kuwa licha ya Uchaguzi wa Kenya kuwa na changamoto lakini zimekuwa nafuu kwa kuwa wana katiba nzuri iliyoifanya tume kuwa huru na kuweza kupinga matokeo ya urais Mahakamani.
Amesema kuwa hatua hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania isingeweza kufikiwa kwa sababu hairuhusu asiyeridhishwa na uchaguzi kwenye hatua ya Urais kwenda Mahakamani kupinga.
“Uchaguzi wa Kenya ulikuwa na changamoto lakini ungekuwa mbaya zaidi kama wengekuwa na Katiba kama yetu,” amesema Henga.
Leave a comment