June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

LHRC chazindua masuala ya katiba mtandaoni

Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba (kulia) akiteta jambo na na Jaji Joseph Warioba

Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), leo kimezindua kanzidata maalumu kwa ajili ya masuala ya Katiba kupitia mtandao wa www.katiba.humanright.or.tz.

Aidha, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa wananchi, wafuatiliaji na watafiti wa masuala ya Katiba kuweza kupata taarifa mbalimbali za masuala ya Katiba zilizokosekana katika hifadhi za taarifa nchini. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi huo Dk. Helen Kijo Bisimba, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho amesema kazi data hiyo ya Katiba imekusanya taarifa mbalimbali kuhusu Katiba toka, kabla na baada ya uhuru.

Amesema imekusanya taarifa za mchakato wa Katiba unaoendelea nchini kwa sasa. Baadhi ya taarifa zinazopatikana ni pamoja na kumbukumbu mbalimbali za kuanzia mwaka 1944 zinazohusu Tanganyika na zile za Bunge Maalum la Katiba.

“Zipo pia taarifa za michakato ya Katiba Zanzibar na Tanzania, Katiba zote za Tanganyika toka mwaka 1920 na kukusanya Katiba zote za Zanzibar na Tanzania toka mwaka 1963 na zile za Tanzania ya sasa,” amesema Bisimba.

Bisimba amesema pamoja na mambo mengine, kanzidata hiyo ina makala mbalimbali za Katiba, sheria, kesi  za kikatiba, taarifa za video, sauti na picha. Taarifa hizo zimegawanyika katika makundi makuu manne, taarifa za; Tanganyika, Zanzibar, Tanzania na nchi nyingine Afrika na duniani.

Aidha, Thomas Mihayo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama Kuu nchini amesema, “…kazi data hii itakuwa kichocheo cha kuhifadhi taarifa si za Katiba tu bali na masuala mengine muhimu ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.”

“Napenda kutoa wito pia kwa waandishi wa habri kukitumia kituo hiki katika makala na tafiti zao mbalimbali, lakini pia kukitangaze ili wananchi wengi wakifahamu na wafaidike. Pia wananchi wakipata taarifa sahihi kwa wakati sahihi, watashiriki kwa kujiamini katika kujua nchi yao na kuielezea kwa mataifa mengine,” amesema Jaji Mihayo.

error: Content is protected !!