KAMPUNI ya LG imetangaza mkakati wake wa 2023 ulioko katika mpango wake wa maendeleo endelevu kufikia 2030, ambao unajumuisha uvumbuzi unaolenga mahitaji ya wateja hususan watu wenye ulemavu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Mkakati huo umetangazwa hivi karibuni katika maonyesho ya CES yanayoendelea jijini Nairobi, Kenya na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, William Cho, akisema kwamba mkakati huo umelenga kujenga maisha bora kwa wateja wake.
“Kampuni ya LG inatazamia kutumia asilimia 100 ya nishati mbadala kufikia mwaka 2025, kupunguza gesi ya ukaa na kuhamasisha mabadiliko ya soko kupitia katika uvumbuzi wake,” imesema taarifa ya LG.
Taarifa hiyo imesema “Akiongea wakati alipokuwa akitangaza maono ya kampuni, Cho alisisitiza utayari wa kampuni wa kuchukua changamoto mpya katika mwaka 2023 na kuendelea bila kujali hali yoyote, ‘akigusia kwamba kampuni ya LG imekuwa inafahamu na kuamini kwa dhati kwamba, jibu liko kwa mteja. Mwanzo na mwisho wa ubunifu wote ni wateja wetu, na ni kwa kupitia ubunifu huu ndipo tunapolenga kuweka tabasamu katika nyuso zao.”
Taarifa hiyo imesema kuwa, ubunifu wa LG kwa 2023 unalenga wateja wa bidhaa zake za umeme za majumbani, pamoja na kufanya kazi na washirika wake kutambulisha aina mbalimbali za huduma kupitia televisheni za LG, ikiwemo mfumo wa elimu kwa njia ya mtandao (MasterClass), program za mazoezi (Max Pro).
“Wakati ambapo inasherehekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa, bidhaa za LG OLED inaendelea kuweka viwango vipya vya ubora katika sekta kwa ubora wa picha na uzoefu wa wateja ambao haujawahi kutokea,” imesema taarifa ya LG.
Leave a comment