Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Letshego yaja na akaunti ya wajasiriamali wadogo, wastaafu
Tangulizi

Letshego yaja na akaunti ya wajasiriamali wadogo, wastaafu

Spread the love

 

TAASISI inayotoa huduma za kifedha nchini Tanzania ya Letshego imezindua akaunti maalum kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wakati na akaunti ya mstaafu kwa ajili ya kuwawezesha kuweka akiba zao kwa malengo ya kuendeleza  biashara zao. Anaripoti Mary Victor, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika leo Jumanne tarehe 27, 2022, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Letshego, Leah Phili, amesema akaunti zilizofunguliwa wamezizindua rasmi kwa wateja wa aina mbili tofauti.

“Tuna kaunti kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo na wakati (Mjasiriamali akaunti), pia tuna akaunti ya wastaafu ambapo akaunti ina jina la mstaafu akaunti. Tukianza na akaunti ya mjasiriamali walengwa wa hii akaunti ni wafanyabiashara wa kati na wadogowadogo kwa hiyo tunafungua akaunti rasmi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza kuweba akiba zao wakiwa na malengo maalum kwenye biashara zao.

Amesema pia wamelenga wateja wadogo wadogo wa chini kabisa ambao hawana nyaraka za kibiashara kama leseni na TIN.

“Kwa hiyo tunachukua mpaka wamachinga na mamalishe, wanaouza biashara ndogo barabarani na ndio walengwa wa hii akaunti,” amesema.

Amefafanua zaidi kuwa akaunti hizo zitawawezesha wafanyabiashara wote kuweza kuhifadhi akiba zao ambazo zitawasaidia kwenye biashara zao na matumizi mbalimbali ya kuhudumia wateja wao na kujihudumia wao wenyewe na familia zao.

Kwa mujibu wa Leah, wamefanikiwa kuondosha baadhi ya vitu ambavyo vitamfanya mteja ashindwe kupata huduma nzuri za kiakaunti.

“Akaunti ya Mjasiriamali unaweza kufungua akaunti kwa shilingi 1000 tu kwa kuanzia, na unaweza kutoa pesa kwenye akaunti yako kwa kiwango cha shilingi 1000 na unaweza kutoa hizo pesa kwa namna mbalimbali, inawezekana kwa kutoa dirishani katika benki zetu, na unaweza kutumia mifumo ya kidigitali mobile bank, na huduma nyingine za kibenki ambazo mteja anaweza akafanya miamala yake kuweka na kutoa.

Leah aliongeza kusema; “Akaunti ile nyingine ya Mstaafu walengwa ni wastaafu na wanaweza kufungua hii akaunti wakati wowote wakiwa wanajiandaa kustaafu na hata baada ya kustaafu pia wanaweza kufungua.

Amesema matumizi makubwa ya akaunti hiyo ni kupitisha fedha zake moja kwa moja kwa ajili ya matumizi yake ya kawaida baada ya kustaafu na mafao yake.

“Sifa kubwa hii akaunti ya Mstaafu haina gharama za mwezi, hii ni akaunti bure, tunamuhudumia mteja bure, hachajiwi hela yoyote kwa ajili ya kuhudumia akaunti yake. Pia anaweza kuweka na kutoa mpaka shilingi 1000,” amesema.

Amesema ku[pitia akaunti hizo wateja wanaweza kupata kadi za VISA au za kawaida za huduma ya switch kwa ajili  ya kufanya miamala na pia wanaweza kuweka na kutoa fedha kupitia simu, mawakala na kadi za ATM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!