February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Leo kila mwathirika MV Nyerere kulamba Mil 1

Spread the love

RAIS John Magufuli anatarajiwa kutoa kiasi cha Shiling milioni moja kwa kila mwathirika wa ajali ya MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana na Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano.

Fedha hizo ni nje ya zile Sh. 500,000 zilizokabidhiwa kwa kila maiti ambapo fedha za leo zitaelekezwa kwa waliofiwa na walionusurika.

“Rais ameniagiza kuwa, ataongeza fedha kwa waathirika na atatoa shilingi milioni moja kwa waathirika wote waliopoteza ndugu zao na walionusurika,” amesema.

Amesema, idadi ya watu waliofariki imeendelea kuongezeka ambapo mpaka kufikia Jumatatu jioni maiti mbili ziliopolewa.

Na kwamba, wahusani wameendelea kuchanga fedha kwa ajili ya msaada kwa waathirika ambapo mpaka Jumatatu jioni likuwa zimeishakusanywa jumla ya Sh. 397 milioni.

error: Content is protected !!