January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lembeli arusha kete Chadema

Mbunge wa Kahama, James Lembeli akizungumza na waandishi wa habari juu uamuzi wake wa kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema

Mbunge wa Kahama, James Lembeli akizungumza na waandishi wa habari juu uamuzi wake wa kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema

Spread the love

JAMES Lembeli, Mbunge wa jimbo la Kahama aliyemaliza muda wake, amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Lembeli amesema ameamua kutochukua fomu na kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM, kwa sababu ya mizengwe inayoendelea ndani ya chama hicho ikiwemo rushwa na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi.

“Kadi nyingi sana zimegawiwa kiholela. Mimi binafsi nimepiga kelele. Wananchi wamepiga kelele. Chama cha CCM kimefunga macho. Chama cha Mapinduzi siyo kibaya. Ila baadhi ya viongozi wake ni watu hatari sana,” amesema Lembeli.

Akithibitisha Lembeli kujiengua CCM na kuhamia Chadema Tumaini Makene, Afisa Habari wa Chadema ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, “..James Lembeli amejiunga na wapiganaji wa Chadema.”

Tumemaliza tukio la kwanza leo. Lembeli baada ya kuwa CCM kimwili kwa muda mrefu huku dhamira yake, uwezo wake, akili zake, zikiwa kwenye mabadiliko ya kweli, leo amekamilisha kile ambacho akili yake ilikuwa inahitaji,”  amesema Makene.

Mbali na Lembeli kujiunga na Chadema, Makene amesema, “…kesho tutawapiga kiaina tena. Keshokutwa pia. Halikadhalika mtondo bila kusahau mtondogoo!.

error: Content is protected !!