July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lembeli apigilia msumari Escrow, tokomeza

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli nje ya viwanja vya Bunge

Spread the love

JAMES Lembeli-Mbunge wa Kahama (CCM), amesema kitendo cha Ikulu kuwasafisha baadhi ya vigogo wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uchotwaji mabilioni ya fedha za escrow na ukiukwaji wa oparesheni tokomeza ni kuipeleka nchi gizani. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).

Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2015/2016 bungeni leo, Lembeli ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, amesema kwa sasa sera ya utawala bora nchini, inatekelezwa kwa ukabila, ukanda na kulindana.

“Mimi nilikuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge iliyochunguza ukiukwaji wa utekelezaji wa oparesheni tokomeza. Katika ripoti yetu tulieleza bayana kwamba wale mawaziri watatu ambao wizara zao zilikuwa na dhamana ya oparesheni hiyo, hawakuhusika moja kwa moja bali waliwajibika kisiasa, sasa nilishanga kuona tena eti serikali inarudia kuwasafisa,” amesema.

Lembeli amehoji “kuna sababu gani ya kusafisha watu hapa akina Eliachim Maswi na Sospeter Muhongo peke yao halafu mnawaacha wengine? Hii ni tabia mbaya.”

Amesema “yuko hapa Lowassa (Edward). Japo mimi sipendi wizi na ufisadi na katika kashfa ya Richmond nilikuwa mmoja wa waliopiga kelele awajibike. Lakini wamesafishwa wengine huyu kwanini naye asisafishwe.”

“Kama ni kufasifishana tusafishwe wote, tuanze upya ndipo nchi hii itatawalika, vinginevyo huko mbele kuna giza nene,” amesema Lembeli.

error: Content is protected !!