June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lema njia panda ukimbizini Kenya     

Godbless Lema

Spread the love

SHIRIKA la kimataifa la kupigania haki za binadamu (Amnest Internatioanal), limeitaka Mamlaka ya Kenya kutofikiria kumrejesha kwa nguvu nchini Godbless Lema, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chadema. Anaripoti Mwa ndishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).  

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 9 Novemba 2020 na kusainiwa na Joanne Kuria, mkuu wa mawasiliano imeonya juu ya uamuzi wa Kenya kuchukua hatua hiyo.

“Amnesty Internation inaonya juu ya uamuzi wa kumrejesha kwa nguvu Tanzania mwanasiasa wa upinzani Godbless Lema ama familia yake,” imeeleza taarifa hiyo.  

Lema aliyekuwa mgombea ubunge Arusha Mjini katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020, amekimbilia nchini Kenya, ili kuomba hifadhi ya kisiasa, katika ubalozi wa Marekani, jijini Nairobi.

Hata hivyo, alikamatwa na Polisi katika Kaunti ya Kajiando baada ya yeye na familia yake kuvuka mpaka wa Namanga, kinyume cha taratibu.

           Soma zaidi:-

Katika Gazeti la The Standard Media, Lema alisema, maofisa wa uhamiaji walikataa kugonga muhuri nyaraka zilizowasilishwa na mke wake, kwa madai hadi wamuone yeye. Alidai, kama angenonesha hati yake ya kusafiria, maofisa hao wangemshikilia na kumzuia kuvuka.

“Nimeacha kila kitu nyumbani. Hivyo havina umuhimu kwa sasa. Muhimu ni usalama wangu na usalama wa familia yangu. Nipo na wanangu Allbless, Brilliance na Terrence. Sijui kesho itakuja na nini. Kwa sasa natafuta hifadhi,” Lema aliiambia The Standard.

Amnesty imeitaka Kenya kuheshimu sheria za kimataifa za ukimbizi wa kisiasa ambazo zinazuia mtu aliyekimbia kutokana na hofu za kisiasa kurejeshwa kwa nguvu.

Godbless Lema, Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema)

“Kenya imezuia kulazimisha kurejesha watu walioomba hifadhi ya kisiasa kwe nye mpaka ama nchi wanayotoka (wanaoomba hifadhi)  kama wanaweza kukabiliwa na hatari,” ameeleza Irungu Houghton, mkurugenzi wa taasisi hiyo kwenye taarifa hiyo.

Hata hivyo, shirika hilo limeeleza, lina imani Lema na familia yake ambao wapo chini ya polisi Kajeri, nchini Kenya watakuwa kwenye mikono salama huku hatua zingine zikiendelea.

Houghton amesema, Lema anayo hadhi ya kupewa hifadhi ya kisiasa na kuendelea kukaa nchini humo mpaka pale utaratibu utakapokamalika wa kumfanya aendelee huhudumiwa kama mkimbizi.

Wakati Lema akisalia nchini Kenya, Tundu Lissu ambaye alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrais  na Maendeleo (Chadema), yuko katika makazi ya balozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam, akiomba hifadhi kwa kile alichoita, “kuhofia” usalama wake.

error: Content is protected !!