HATIMAYE Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema, ametangaza kurejea nchini tarehe 3 Machi 2023. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam …(endelea).
Lema ambaye anaishi nchini Canada tangu mwaka 2020 ambapo alitimkia huko baada yauchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba, anatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Lema ameandika; “Ndugu, rafiki, jamaa, wanachama, wananchi na viongozi wenzangu. Tukutane KIA Tarehe 1/3/2023 Saa 6 Mchana.”
Aidha, Lema ameeleza kuwa baada kupokewa, ataelekea jijini Arusha kwa ajili ya mkutano wa hadhara kama alivyofanya Tundu Lissu – Makamu Mwenyekiti wa Chadema.
“Kisha tutaondoka kuelekea Arusha ambako kazi ya kupulizia sumu chawa na makazi yao itaanza mara moja. Chawa ni wadudu wachafu ninakuja na sumu kali kutoka nchi za Magharibi” aliandika Lema.
Huyu ni kiongozi wa pili Chadema anayerejea nchini ikiwa ni siku chache zimepita tangu Lissu ambaye alikuwa anaishi nchini Ubelgiji kurejea tarehe 25 Januari 2023.
Aidha, kada mwingine wa Chadema aliyepo nje kwa madai kuikimbia nchi kutokana na madhila ya kisiasa ni Mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekiel Wenje aliyepo nchini Marekani.
Leave a comment