July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lema atibua, Bunge laahirishwa

Spread the love

HOTUBA ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imezuia, anaandika Faki Sosi.

Bunge limeahirishwa mpaka saa 10 jioni baada ya kuzuia kusomwa kwa hotuba hiyo kwa madai kwamba, ina maneno yanayohitajika kuondolewa ili ikidhi matakwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Kanuni.

Ndani ya Hotuba ya Lema (Mwanahalisi Online inayo) kipo kipengelea kinachoelezea sakata la makataba tata wa Kampuni ya Lugumi ambapo Kamati ya Mambo ya Ndani ilielezwa suala hilo kutojadiliwa bungeni kwa madai tayari lilikuwa limeanza kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Kipengele kinachohusu mkataba wa Kampuni ya Lugumu kipo kwenye sehemu ya tano inayoeleza Mikataba Tata ya Jeshi la Polisi.

Kwa muda mrefu mkataba huo uliotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd wenye thamani ya Sh 37 bilioni umedaiwa kuwa na harufu ya ufisadi.

Mwaka 2011, kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kufunga mashine za alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini na kulipwa Sh 34 bilioni kati ya Sh 37 bilioni sawa na asilimia 99 ya malipo yote.

Mkataba huo umeonekana kuwa na utata mkubwa na kusababisha sintofahamu kutokana na kukosekana kwa maelezo yaliyonyooka.

error: Content is protected !!