ALIYEKUWA Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amepata hifadhi ya ukimbizi ya kisiasa nchini Canada. Anaripoti Mwandishi Wetu, Nairobi … (endelea).
Lema aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kati ya mwaka 2010-2020, ameondoka jana Jumatano tarehe 9 Desemba 2020 kwenda Canada yeye pamoja na familia yake akitokea jijini Nairobi nchini Kenya.
Lema alikuwa Kenya tangu tarehe 8 Novemba 2020 alipokwenda nchini humo kwa lengo la usalama wake baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu uliofanyika 28 Oktoba 2020, yeye akiwa mgombea wa Arusha Mjini.
Hata hivyo, Lema alishindwa kwenye uchaguzi huo na Mrisho Gambo wa Chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mara baada ya kuingia Kenya, alikamatwa kwa kile kilichoelezwa ni kuingia pasina kufuata taratibu. Hata hivyo, aliachiwa ili kuendelea na taratibu za kutafuta hifadhi ya kisiasa.
Picha mbalimbali zimemwonyesha Lema akiwa na familia yake (mke wake , Neema na watoto wake watatu) pamoja na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe muda mfupi kabla ya kuondoka Kenya kwenda Canada.
Katika ukurasa wake wa facebook, Lema ameweka picha hizo na kuandika ‘We shall meet again’ akiwa na maana ‘tutaonana baadaye.’
Asante asiye sikia la mkuu uvunjika ameewafata wakolon sio vibaya kichungu uwonja