August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lema aachwa gizani, Zitto ampa nguvu

Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, akirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana

Spread the love

MSIOGOPE. Ni kauli ya Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini aliyoitoa baada ya Engelo Rumisha, Naibu Msajili wa Mahakama ya Kuu Kanda ya Arusha kumwacha ‘gizani,’ anaandika Mwandishi Wetu.

Naibu Msajili huyo alimwacha kwenye mshangao muda mchache baada ya kumpa nafasi Lema kuzungumza na wakili wake wakati wa kesi hiyo.

Hatua ya Naibu Msajili huyo kumwacha Lema gizani ilitokea baada ya kuwepo kwa mabishano makali baina ya mawakili wa Lema na Naibu Msajili huyo.

Mzozo ulianza baada ya wafuasi wa Lema kuzuiwa kuingia katika lango kuu la mahakama hiyo, wafuasi hao walitaka kwenda kusikiliza nini kinaendelea wakati ambao mawakili wa mbunge huyo wakiendela kuangaikia rufaa ya mteja wao (Lema).

Lema alifikishwa kwenye mahakama hiyo tarehe 29 Agosti mwaka huu na kusomewa mashtaka mawili;
La kwanza akidaiwa kutuma ujumbe wa kuudhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo unaosema ‘karibu Arusha tutakudhibiti kama Arabuni wanavyodhibiti mashoga’.

La pili akidaiwa kutuma ujumbe wa sauti kwenye mitandao unaohamasisha maandamano yasiyokuwa na kibali.

Kwenye kesi hilo Lema anatetewa na John Malya, Peter Kibatala, Faraji Mangula, Adam Jabir na Sheki Mfinanga wakati Jamhuri ikiwakilishwa na mawakili waandamizi Matrenus Mrandu na Paul Kadushi.

Hata hivyo, baada ya kuibuka mzozo huo, Lema aliomba ruhusa kwa kunyoosha mkono akitaka kuzungumza.

Mbunge huyo alianza kunyoosha mkono kabla hata Naibu Msajili kuanza kusoma uamuzi wa rufaa yake, hata hivyo Naibu Msajili alikataa kumpa ruhusa ya kuzungumza kwa kumwambia ‘anao mawakili wake.”

Na baada ya Naibu Msajili kusoma uamuzi, alimweleza Lema kwamba, kama anataka kuzungumza, sasa anaweza kufanya baada ya kutoka pale alipo.

Uamuzi wa Naibu Msajili ulipokewa kwa mikono miwili na Lema pia mawakili wake ambapo walisimama na kuanza kuzungumza.

Lakini wakati Lema na mawakili wake wakiteta, ghafla Naibu Msajili alisimama na kusema kuwa amemaliza kesi.

Baada ya kauli yake hiyo, alitoka kwenye chumba cha mahakama hiyo ya wazi jambo lililowaduwaza Leman na mawakili wake huku wakishindwa kujua nini cha kufanya.

Hatua hiyo pia iliwashangaza watu wengine waliokuwa wamehudhuria kusikiliza kesi hiyo, hata hivyo, baada ya kutokea tukio hilo, Lema aliwataka kuendelea kujipa moja na kuondoa woga.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalengo aliyekwenda kumtembelea Lema kwenye Gereza la Kisonge jijini humo na amesema kuwa, amempa ujumbe Lema kwamba, mapambano hayo si yake peke yake na kwamba, wapo wengi nyuma yake.

Zitto amesema kuwa, yupo pamoja na mbunge huyo wa Arusha na kwamba, ujuo wake kwenye gereza hilo, ni kumtembelea mbunge mwenzake.

Hata hivyo, ameeleza kumnasihi Lema kwamba, awatazame mahabusu wengine wanaoteseka gerezaji bila kesi zao kuendelea na awatetee.

error: Content is protected !!