August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Leicester City timu bora ya mwaka

Kikosi cha Leicester City cha mwaka 2015/16

Spread the love

KLABU ya Leicester City inayoshiriki Ligi Kuu England imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka baada ya kutwaa ubingwa nchini humo, huku kocha mkuu wa timu hiyo Claudio Ranieri akitangazwa kuwa Kocha Bora wa Mwaka baada ya kuisaidia timu kushinda taji katika msimu uliomalizika.

Leicester ilianza harakati za kusaka ubingwa huo toka ilipopanda daraja katika msimu wa 2014/15, na msimu mmoja baadae walifanikiwa kuchukua ubingwa ambao ulikuwa wa kwanza katika historia ya klabu hiyo baada ya kupoteza michezo mitatu katika mechi 38 walizocheza msimu mzima.

Licha ya ubingwa huo lakini kilichowashangaza wengi ni aina ya kikosi alicho kuwa nacho Raniel, kwani kilikuwa na wachezaji wa kawaida ambao thamani na ubora wao haukuwa mkubwa.

Kikosi hicho ambacho kilimpa ubingwa Raniel katika msimu uliomalizika hakijabadilika kwa asilimia kubwa na kikosi kinachoshiriki ligi hiyo sasa na michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ambao wamefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora baada ya kuwa vinara katika kundi G.

Lakini mwendendo wa sasa kwenye ligi unawashangaza wengi ambapo mpaka sasa inashika nafasi ya 17 na huku ikiwa na alama 17 baada ya kushinda michezo minne, kupoteza nane na kwenda sare mara tano huku kwenye kikosi hicho akiwa amepungua Ngolo Kante ambaye ametimkia kwenye klabu ya Chelsea mwanzo wa msimu.

error: Content is protected !!