Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza viwango vya nauli mpya za daladala na mabasi ya kwenda mikoani. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Viwango hivyo vimetangazwa leo Jumamosi Tarehe 30, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe, wakati akizungumza na waandishi wa Habari.

Ngewe amesema viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika baada ya siku 14.

Kwa nauli za mikoani amesema mabasi ya daraja la kawaida kwa kwa kilometa 1 imeongezeka kutoka Sh. 36 kwa kilometa moja hadi Sh. 41.

Kwa daraja la kati imeongezeka kutoka Sh. 53 kwa kilometa moja hadi Sh56.88.

Ameongeza kuwa kwa mabasi ya mjini kuanzia kilomita 0 hadi 10 nauli itakuwa Sh. 500 badala ya Sh. 400 na nauli ya Sh. 450 itakuwa Sh. 550.

Amesema kuwa kwa kilomita 30 nauli itakuwa Sh. 850 badala ya Sh. 750 na kwa kilometa 35 nauli itakuwa Sh. 1000 huku kilometa 40 ikiwa ni Sh.1100.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *