Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko LATRA yafunguka chanzo BOLT kusitisha usafiri wa magari
Habari MchanganyikoTangulizi

LATRA yafunguka chanzo BOLT kusitisha usafiri wa magari

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema mojawapo ya sababu ya baadhi ya Kampuni za teksi mtandaoni kusitisha huduma za usafiri wa magari ni kutoridhika na kiwango elekezi cha asilimia 15 kutoka katika mapato ya dereva  kwenda kwa kampuni hizo kama kamisheni. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea)

LATRA imetoa ufafanuzi huo baada ya Kampuni ya teksi mtandaoni – BOLT kutangaza kusitisha huduma za usafiri wa magari yanayopokea pesa taslimu kuanzia leo tarehe 17 Agosti, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LATRA jana tarehe 16 Agosti, 2022 imesema mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria namba 3 ya mwaka 2019 ilitangaza viwango vya nauli za teksi mtandao kupitia Gazeti la Serikali namba 1369 la tarehe 8 Aprili, 2022 na vyombo vya habari.

“Pamoja na viwango vya nauli za teksi mtandao, Mamlaka iliweka kiasi cha ukomo wa makato ya asilimia 15 kutoka katika mapato ya dereva kwenda kwa kampuni za teksi mtandao kama kamisheni.

“Hata hivyo, baadhi ya kampuni za teksi mtandao zilizokuwa zikitoza kamisheni ya asilimia 20 mpaka 31 hazikuridhika  na kiwango elekei cha asilimia 15.

“Kampuni zingine za teksi mtandao zikiwemo Little Ride, Paisha na Ping zimeridhia na zinaendelea kutoa huduma kwa viwango vya nauli na kamisheni vilivyoidhinishwa na mamalaka,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, imesema kutokana na baadhi ya kampuni hizo kusitisha huduma ikiwamo BOLT, imewashauri abiria na madereva wa teksi mtandao kuwa kutumia kampuni hizo Little Ride, Paisha na Ping zilizoridhia wakati inandelea kushughulikia changamoto za huduma za teksi mtandao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

error: Content is protected !!