July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lamudi wawataka wananchi kupima ardhi zao

Meneja Mkazi wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa akizungumza na waandishi wa habari

Spread the love

KAMPUNI ya Lamudi Tanzania imewataka wananchi wa Tanzania kuwa na utamaduni wa kupima ardhi zao ili kuepuka migogoro ya ardhi pamoja na kutambulika maeneo yao katika ramani ya Taifa, anaripoti Erasto Stanslaus.

Kampuni hiyo inayojishughulisha na uuzaji wa mali zisizohamishika imetoa kauli hiyo ikiwa ni kuwaunga mkono Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mkakati wake wa kuhakikisha maeneo yote yanakuwa katika vipimo.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Meneja Mkazi wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa alisema wamiliki wa ardhi anatakiwa kuwa na utamaduni wa kupima ardhi yake ili kukwepa migogoro ambayo inaweza kujitokeza siku za usoni.

Nyagawa alisema Wizara imekuwa na jitihada kubwa kuhakikisha kila anayemiliki ardhi awe ameipima lakini bado elimu hiyo haijaeleweka vizuri na wananchi.

“Wizara katika bajeti ya mwaka huu, wamejitahidi kununua mashine ya kisasa ya kupimia ramani ya ardhi na wameanza kwa Dar es Salaam, lakini changamoto wanayokutana nayo ni kutopimwa kwa maeneo mengi ya jiji hilo. Elimu zaidi inatakiwa kutolewa ili kufanikiwa adhimio la wizara,” alisema Nyagawa.

Aliongeza kuwa mbali na tatizo la wananchi kutopima viwanja vyao, pia kuna changamoto ya viwanja vilivyopimwa kiholela.

Meneja huyo wa Lamudi, aliwataka wananchi kuwa makini wanapohitaji kununua viwanja au nyumba, kwani wanatakiwa kununua maeneo ambayo yamepimwa na ramani yake inatambulika wizarani.

Lamudi pamoja na wizara husika inapendekeza kuwepo kwa sheria ya kupima maeneo ambayo itamfanya kila mwananchi apime ardhi yake ili kuepuka migogoro ya ardhi kama iliyotokea Mabwepande, Morogoro na maeneo ya wakulima na wafugaji.

error: Content is protected !!