July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lamudi watoa somo kwa wanunuzi wa viwanja, nyumba

Meneja wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa

Spread the love

KAMPUNI ya Lamudi Tanzania imetoa somo kwa wanunuzi wa mali zisizohamishika kama viwanja au nyumba kwa wateja ili kuepukana na matapeli wa uuzwazi wa mali hiyo kuongezeka kwa kasi. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Kasi ya ongezeko la watu binafsi na mashirika yanayojenga nyumba za biashara, imesababisha kuongezeka kwa utapeli wa nyumba na viwanja visiyohalali.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Meneja wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa alisema Lamudi imeamua kutoa somo hilo kwa lengo la kuwatahadharisha Watanzania kutotapeliwa na matapeli waliopo katika soko la mali zisizohamishika.

Nyagawa alisema Lamudi wameainisha njia kuu tatu za kuzingatia kabla ya kununua au kupanga mali isiyohamishika. Njia hizo kuu tatu ni hizi hapa chini:-

1. Hakikisha nyumba au kiwanja ina Hati miliki.

Hati ya nyumba au kiwanja ni lazima iwe inatambulika na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Lamudi Tanzania inashauri kwa wateja wote hata wenye lengo la kupanga wahakikishe wanaona hati miliki ya mtu anayempangisha ili kuepuka utapeli wa kupangishwa na mtu asiyehusika.

2. Mwanasheria na shahidi.

Kuna baadhi ya wateja wanasahau umuhimu wa mwanasheria na kuona suala la kupanga au kununua ni jambo la mazoea. Mwanasheria anasaidia hasa kama mali inayouzwa siyo halali, hivyo inakuwa si rahisi mtu kukuuzia akiwa na lengo la utapeli.

Mwanasheria pia husaidia kuelewa mkataba vyema iwapo utahitaji ufafanuzi wowote kuhusiana na mkataba. Mbali na mwanasheria lakini pia shahidi ni mtu muhimu, ambaye anasimama kama mtetezi iwapo utatokea utapeli wowote.

3. Hakikisha unatambua historia ya sehemu unayotaka kuishi au kununua.

Wateja wengi huwa wanasahau kufatilia historia ya sehemu anayotaka kupanga au kununua, wengi wetu huwa tunatazama bei na ubora wa nyumba au kiwanja anachohitaji, lakini kihistoria viwanja vingine huwa na migogo ya kifamilia au serikali na jamii.

Wakati huo huo, Afisa Masoko na Mahusiano ya Jamii wa Lamudi Tanzania, Lilian Kisasa aliwataka Watanzania pamoja na kuzingatia hatua hizo tatu lakini Watanzania wanatakiwa kuzingatia hati miliki na mikataba ya mali wanazonunua kabla ya kununua.

error: Content is protected !!