July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lamudi watangaza utalii wa Tanzania

Bonde la Ngorongoro

Spread the love

KAMPUNI ya Lamudi Tanzania imewahimiza Watanzania kutembelea katika maeneo ya Utalii ikiwa ni sehemu ya kutangaza maeneo yenye vivutio.

Lamudi imejitolea kutangaza maeneo ya kuvutia ndani ya Tanzania ambayo familia zinaweza kutembelea wakati wa sikukuu ya sherehe mbalimbali.

Maeneo ambayo Watanzania wanaweza kutembelea katika sikukuu ni kama zifuatazo.

Visiwa vya Zanzibar

Zanzibar ni moja kati ya sehemu zenye vivutio ambavyo Watanzania wanaweza kupata burudani wakiwa katika sehemu hizo.

Watalii wakiwa Zanzibar watapata fulsa ya kutalii kwenye fukwe safi zilizopoa pembezoni mwa bahari, lakini pia watapata nafasi ya kutembelea kwenye mji wa mawe ‘Stone town’.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Mbuga za wanyama za Serengeti ni sehemu sahihi kwawatalii wa ndani kutembelea kutokana na kuwa na vituvio vya kila aina hasa wanyama wa aina zote.

Mbuga hiyo yenye ukumbwa wa kilomita za mraba 14,763 zinazompa mtalii nafasi za kutembea kwa muda mrefu, sifa nyingine ya mbuga hiyo ni uwepo wa hoteli zenye hadhi ya nyota tano.

Mlima wa Mahale

Milima ya Mahale yana sifa kubwa ya kuwepo kwa nyani wekundu na nyani wa njano ambao hawapatikani sehemu nyingine yoyote duniani.

Mbali na nyani hao lakini mtalii akitembelea kwenye milima hiyo, atapata fulsa ya kupamba mlima huo lakini pia kutalii kwenye maporomoko ya mali kwenye mlima huo yanayodondokea kwenye Ziwa Tanganyika. Ukiwa kwenye milima hiyo utaweza kufikia Greystoke Mahale au Nkungwe Tented Camp

 Ziwa Victoria

Sifa kubwa ya Ziwa Victoria ni kuunganisha nchi tatu za Afrika Mshariki, Kenya, Uganda na Tanzania, mtalii akiwa kwenye ziwa hili atapata fulsa ya kutembelea visiwa vilivyo kwenye ziawa hili sambamba na uvuvi wa samaki.

Pamoja na ziwa hilo kuwa sehemu ya maji lakini pia kuna visiwa vya utalii kama Kisiwa cha Rubonda ambacho kina wanyama wa aina mbalimbali.

Bonde la Ngorongoro

Olduvai Gorge iliyopo ndani ya Ngorongoro ni sehemu muhimu na ya kipekee kwa Tanzania kwani ndiyo sehemu ambayo mabaki ya binadamu wa kwanza yaligunduliwa, watanzania wanaweza kutembelea hapo ili wapate kujua zaidi.

Mbali na kumbumbuku hiyo muhimu lakini pia mbuga hizo kuna wanyama wa kila aina lakini wakiwemo faru na simba wakubwa zaidi nao wanapatikana kwenye mbuga hiyo.

Lamudi Tanzania inawahamasisha Watanzania wakipata fulsa ya kupumzika wanatakiwa kufikiwa sehemu moja kati ya hizo, kwa lengo la kupata mapumziko lakini poa kuiongozea kipato Serikali kupitia utalii.

error: Content is protected !!