December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lamudi: Wanawake waamka kumiliki ardhi

Wafanyakazi wa kike wa Lamudi Tanzania

Spread the love

WANAWAKE wa kampuni ya Lamudi Tanzania wanaungana na wanawake duniani kote kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa leo, huku wakishuhudia ongezeko la wanawake wanaomiliki ardhi na mali zisizohamishika wakiongezeka.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanawake wa Lamudi Tanzania, wamesema kuwa wanasherehekea siku ya Wanawake Duniani kwa faraja kutokana na idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi na mali zisizohamishika wameongezeka.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano na Masoko wa Lamudi Tanzania, Masserat Alarkhia ameliambia MwanaHALISI Online kuwa idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi na mali zisizohamishika imeongezeka tofauti na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Naye Afisa Uhusiano na Masoko wa Lamudi Tanzania, Lilian Kisasa amesema muamko wa wanawake katika kumiliki ardhi na mali zisizohamishika umekuwa kwa kasi, lakini pia hawapo nyuma katika kukua na kuongeza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Kemilembe Ramadhani ambaye ni Afisa Uhusiano na mitandao ya kijamii wa Lamudi Tanzania, amewataka wanawake nchini kutokuwa nyuma katika kumiliki ardhi na mali zisizohamishika kwani hazipo kwa wanaume pekee.

Meneja Masoko wa HassConsult Real Estate ya Kenya, Sakina Hassanali amesema nchini Kenya mali zisizohamishika na ardhi zilikuwa zikimilikiwa na wanamume lakini sasa hali imebadilika wanawake wengi sasa wanamiliki mali hizo.

Wanawake wengine wa Lamudi kutoka katika nchi tofauti tofauti waliotuma salamu za Sikukuu ya Wanawake Duniani ni pamoja na Claudia Silva wa Colombia, Yodit Abera wa Ethiopia, Saida Filali wa Morocco, Wafa Umer wa Pakistan, Charm May Thu wa Myanmar na dalali maarufu nchini, anayetambulika kama Dalali Mwanamke.

Lamudi Tanzania inawatakiwa wanawake wote wa heri ya Sikukuu ya Wanawake Duniani.

error: Content is protected !!