May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lampard kuwashiwa taa ya kijani Chelsea

Frank Lampard

Spread the love

 

TAARIFA kutoka vyanzo mbalimbali nchini Uingereza vinasema huwenda muda wowote klabu ya Chelsea ikamtimua kocha wake wa sasa Frank Lampard kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni na nafasi yake itachukuliwa na kocha wa zamani wa PSG, Thomas Tuchel. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tuchel ambaye pia alikuwa kocha wa zamani wa klabu ya Borrusia Dortmund taarifa zinaeleza kuwa tayari yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa klabu ya Chelsea kuja kuchukua mikoba ya Lampard ambaye muda wowote ataondoka klabuni hapo.

Lampard ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ataondoka kwenye klabu hiyo kutokana na kuwa na mwenendo mbovu wa matokeo kwenye michezo ya Ligi Kuu nchini England.

Mpaka sasa Lampard ameingoza Chelsea kwenye michezo 83 katika kipindi cha miezi 18, toka alipojiunga na klabu hiyo msimu uliopita.

Mpaka sasa Chelsea ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi hiyo mara baada ya kucheza michezo 19 na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo nane, huku akipoteza mechi sita na kwenda sare michezo mitano.

error: Content is protected !!