Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Lampard astaafu soka
Michezo

Lampard astaafu soka

Frank Lampard
Spread the love

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Chelsea, New York City FC na timu ya taifa ya England, Frank Lampard (38) leo ametangaza kustaafu mchezo wa mpira wa miguu baada ya kuucheza kwa mafanikio katika kipindi cha miaka 21, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Lampard ambaye mpaka anatangaza kustaafu soka ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England, mataji mawili ya Kombe la Ligi, mataji matatu ya kombe la chama cha soka nchini England (FA) na taji la Klabu Bingwa Ulaya mara moja.

Mkongwe huyo ametangaza uamuzi wake wa kustaafu soka kupitia kwenye ukurasa wake unaopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuandika waraka mrefu kwenda kwa washabiki zake na wapenzi wa soka wote ulimwenguni.

Lampard aliandika kuwa huu ndio wakati sahihi wa yeye kustaafu mpira licha ya kupokea ofa nyingi ili aendelee kucheza mpira.

“Baada ya miaka 21 ya kucheza mchezo wa soka, sasa nimeamua kwamba ni wajati muafaka wa kustaafu mpira kama mchezaji wa kulipwa.”

“Wakati huo nimepokea ofa nyingi na nzuri kutoka nyumbani na nje ya nchi ili niendelee kucheza mpira, lakini kwa umri huu wa miaka 38 najisikia sasa ni wakati wa kuanza sura mpya katika maisha yangu,” aliandika Lampard kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mpanga anatangaza kutundika daruga, Lampard amecheza jumla ya michezo 106 katika timu ya taifa, na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Chelsea baada ya kufunga mabao 211 kwa mashindano yote aliocheza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

Michezo

Jumamosi ni zamu yako kufurahia mkwanja na Meridianbet

Spread the loveWikendi ndiyo hii imefika jaman na wewe kama mteja wa...

error: Content is protected !!