Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa LAAC yabaini ‘madudu’ Chemba na Chamwino, yampa rungu CAG
Habari za Siasa

LAAC yabaini ‘madudu’ Chemba na Chamwino, yampa rungu CAG

Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeishauri Ofisi ya Mthibiti na Mgamuzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu kwa halmashauri ya Chemba na Chamwino zote za mkoani Dodoma. Anaripoti Danson Kaijade, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa tarehe 13 Agosti 2021 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Grace Tendega alipokuwa akitoa taarifa ya majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendelo katika wilaya ya Chemba na Chamwino kutokana na miradi yao kutoridhisha.

Amesema kamati imetembelea miradi mbalimbali katika halmashauri tatu katika Mkoa wa Dodoma ambazo ni Chemba, Mpwapwa na Chamwimo.

Akizungumzia Wilaya ya Chemba kamati imesema imebaini kuwepo miradi ambayo imetekelezwa chini ya kiwango.

“Kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na ununuzi wa samani kwa ajili ya madarasa hayo kwa thamani ya milioni 40 lakini mradi huo hauna viwango vinavyokubalika.”

“Kamati imebaini licha ya madarasa hayo kutoanza kutumika lakini tayari sakafu imeishaanza kubanduka jambo ambalo linaonesha hapakuwa na usimamizi madhubuti na masuala ya kiufundi kutokuzingatiwa hivyo kuruhusu ujenzi kutokuwa na viwango vya ubora.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

“Kuhusu idadi ya takwa kila darasa hairuhusu watoto kusoma nyakati za usiku” amesema Tendega.

“Kutokana na hali hiyo kamati imeagiza halmashauri kutumia pesa zake za ndani kuimarisha sakafu na kuweka taa kabla ya mwezi Desemba mwaka huu,”amesema Tendega.

Kuhusu halmashauri ya Chamwino amesema, kamati imetembelea mradi wa hospitali ya Mlowa barabarani pamoja na ujenzi wa madarasa mawili na vyoo lakini majengo hayo yapo chini ya kiwango.

“Pamoja na kuwa chini ya kiwango kamati imebaini kuwa hakuna mchanganuo mzuri wa matumizi ya fedha kutoka serikali kuu pamoja na nguvu za wananchi.”

“Kutokana na hali hiyo kamati imeagiza ofisi ya CAG kufanya ukaguzi maalumu ili kubaini matumizi sahihi ya utekelezaji wa miradi hiyo,”ameeleza Tendega.

Kwa upande wa halmashauri ya Mpwapwa wameshauri Tamisemi kuona uwezekana wa kuongeza fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi kama sehemu kitegauchumi.

Kwa upande wa Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema kuwa anakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya kutaka Chamwino na Chemba kufanyiwa ukaguzi maalumu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!