Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu La sita, la tano wasoma chumba kimoja
Elimu

La sita, la tano wasoma chumba kimoja

George Simbachawene, Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Spread the love

WANAFUNZI wa shule ya msingi Magwalisi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wanatumia chumba kimoja, kwa wakati mmoja wakati wa kufundishwa wanafunzi wa madarasa wa ngazi tofauti kutokana na uchache wa vyumba vya madarasa, anaandika Esther Macha.

Jonathan Chengula, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema kuwa shule yao ina vyumba vinne tu vya madarasa, hali ambayo inawapa ugumu wakati wa ufundishaji wa wanafunzi.

“Tungeweza kuchangiwa na wazazi tukaongeza madarasa hata hivyo, shule ipo kwenye mgogo na inadaiwa kuwa ndani ya mipaka ya Mamlaka ya Hifadi ya Taifa (TANAPA), hivyo wazazi wanahofia kuongeza vyumba vya madarasa kisha shule ije kuhamishwa,” amesema Chengula.

Wema Amosi, mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo, amesema; “Tunaiomba serikali ituongezee majengo mengine ili tuweze kumudu masomo ambayo tunafundishwa darasani, tukiongezewa vyumba vya madarasa itakuwa msaada mkubwa kwetu.”

Clemencia Kitalima, mwanafunzi mwingine wa darasa la sita, amesema uchache wa vyumba vya madarasa umekuwa ukipelekea chumba kimoja kusomea wanafunzi wa madarasa mawili hali ambayo inaawathiri wanafunzi hao kutokana na kutosoma kwa nafasi.

“Tunaingia chumba kimoja ingawa sisi ni madarasa mawili tofauti kwahiyo tunageuziana migongo na walimu wawili tofauti wanatufundisha,” amesema.

Goden  Mgombavanu, mwenyekiti wa kitongoji cha Nyalunga, ilipo shule hiyo amemwambia mwandishi wa habari hii kuwa, changamoto kubwa iliyopo ni mgogoro wa mipaka ya Tanapa,  hivyo kushindwa kuendelea na ujenzi kwa hofu ya kuja kuhamishwa.

“Ni kweli, shule hii ina vyumba vichache na watoto wetu wanateseka hivyo ni vema serikali ikaliona hili ili mipaka halisi ya shule uweze kufahamika na wazazi waweze kuendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa gharama zao,” amesema Mgombavanu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

Elimu

Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto

Spread the love  SHULE ya Sekondari ya Alpha ya jijini Dar es...

error: Content is protected !!