Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Michezo La Liga yanoga, Benzema aweka rekodi Madrid
Michezo

La Liga yanoga, Benzema aweka rekodi Madrid

Karim Benzema
Spread the love

 

LIGI kuu ya Hispania maarufu kama ‘La liga Santander’ jana tarehe 22 Septemba imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali huku mshambuliaji wa Madrid, Karim Benzema akiendelea kusimika ufalme wake nchini humo. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo … (endelea).

Katika michezo ya jana vilabu mbalimbali vilimenyana ambapo Real Madrid ilipata ushindi mnono wa bao 6-1 dhidi ya Mallorca, Sevilla alishinda 3-1 dhidi ya Valencia, Espanyol wakipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Deportivo Alaves na Villareal waliwachakaza Elche bao 4-1.

Aidha, katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Mallorca, Staa wa timu hiyo Karim Benzema aliendeleza ubabe baada ya kutupia kambani mabao mawili na kutoa pasi mbili za mwisho zilizozaa mabao mawili.

Hata hivyo, bao lake moja likikataliwa na muamuzi wa mchezo huo, huku mchezaji mwenzie Marco Asensio akifunga mabao matatu yaani ‘Hat trick’ na Isco akifunga bao moja.

Baada ya mchezo huo Benzema kwa sasa ndiye kinara wa mabao katika ligi hiyo ya Hispania akiwa na idadi ya mabao sita na kuweka rekodi ndani ya klabu ya Real Madrid kwa kufikisha idadi ya mabao 200 .

Ikumbukwe kuwa Benzema ni miongoni mwa wafungaji 10 wa muda wote kuwahi kutokea katika klabu hiyo akishikilia nafasi ya 5 huku Cristiano Ronaldo akiwa mfungaji mkuu wa muda wote katika klabu ya Real Madrid.

Michezo mingine itakayochezwa leo ni pamoja na Granada dhidi ya Real Sociedad, Osasuna atakipiga na Real Betis huku Cadiz itakiwasha na Barcelona.

Mpaka sasa Madrid wanashika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Atletico Madrid katika nafasi ya pili huku Barcelona akiwa nafasi ya nane pamoja na mechi mbili mkononi ikiwamo ya leo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

error: Content is protected !!