December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kwanini serikali inalipisha fedha maiti?-Mbunge ahoji

Spread the love

MBUNGE wa upinzani ameitaka serikali ieleze, ni lini itaacha kulipisha fedha maiti? Anaripoti Danson Kaijage … (endelea).

Ni kutokana na mgonjwa kufia hospitalini wakati akitibiwa.

Swali hilo limeibuliwa leo tarehe 6 Septemba 2019 bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo (Chadema) alipokuwa akiuliza swali la nyongeza juu ya utozwaji fedha kwa wafiwa ambao wanashindwa kulipa ili kukomboa maiti.

Akiuliza swali la nyongeza Lyimo alihoji na kutaka kujua, ni lini serikali itaachana na tabia ya kuwatoza fedha wananchi ambao wanapoteza ndugu zao wakati wakitibiwa na ukizingatia wananchi wengi hawana uwezo?

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua serikali itaacha gharama miili ya marehemu hospitalini na kuifadhiwa katika vyumva vya kuifadhia maiti ili kupunguza simanzi kwa wafiwa.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto,Dk.Faustine Ndugulile alisema kuwa kwa Mujibu wa sera ya Afya ya mwaka 2017 wananchi wanatakiwa kuchangia gharama za afya ikiwa ni pamoja na matibabu na hata huduma za kuifadhi maiti.

Alisema, inapotokea mwananchi anakabiliwa na changamoto ya kushindwa kumudu gharama za uhifadhi wa maiti, mwananchi huyo anatakiwa kutoa ripoti kwenye uongozi wa hospitali husika ili kupata maelekezo ya namna ya kutatua changamoto hiyo.

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya amesema, ili kuondokana na changamoto hiyo, ni vyema kujiunga na Bima ya afya.

Hata hivyo, amesema kuwa serikali imeweza kutoa msamaha kwa wananchi wengi ambao wamekuwa wakikalibilwa na changamoto ya kushindwa kulipia gharama za maiti.

Amesema, siyo sahihi kuwa kinacholipiwa ni mwili wa maiti bali ni gharama za dawa ambazo zinatumika katika kumpatia matibabu.

error: Content is protected !!