August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kwanini Putin anamzimikia Trump?

Spread the love

VLADMIR Putin, Rais wa Urusi amesema kuwa, anamuunga mkono Donald Trump, rais mteule wa Marekani kwa kuwa ndiye pekee anayeweza kurejesha uhusiano wa taifa lake na Marekani, anaandika Wolfram Mwalongo.

Hata hivyo Putin ameonesha hofu ya kufanikisha azma hiyo kutokana na tofauti ya kimisimamo baina ya mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa katika mvutano mkubwa hususani katika kurejesha amani nchini Syria.

Amesema kwamba, hakati tama na kuwa atafanya kila analoweza kuhakikisha machakato wa uhusiano mwema kati ya Marekani na Urusi unakamilika.

Wakati Putin akijiegemeza kwa Trump kama karata yake muhimu katika kutimiza azma hiyo, Marekani imeendelea kuituhumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi mkuu uliopita na kwamba, ilikuwa ikidukua tarifa kwenye Komputa za Chama cha Democratik.

Kitendo hicho kinatajwa kama sababu iliyochangia kuanguka kwa mgombea wake Hillary Clinton aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Obama amelitaka Shirika la Ujasusi (CIA) kwa kushirikiana na Shirika la Upelelezi (FBI) nchini mwake (CIA) kufanya uchunguzi juu ya udukuzi huo.

Taarifa za awali zilizotolewa na CIA wiki ilipita zinasema kwamba, kwa asilimia 90 Urusi ilishiriki katika njama hizo za kisiasa ingawa uchunguzi zaidi unaendelea.

Uhusiano wa mataifa haya mawili umekuwa wa mashaka kutokana na kwamba Urusi imekuwa ikipuuza makatazo ya Marekani ya kuzuia uzalisha wa silaha za Nyuklia huku Marekani ikituhumiwa kutengeneza sila hizo kwa kificho.

error: Content is protected !!