Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kwanini Maalim Seif apewe kadi No. 1 ACT-Wazalendo?
Habari za Siasa

Kwanini Maalim Seif apewe kadi No. 1 ACT-Wazalendo?

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamadi, mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 19 Machi 2019 amekabidhiwa kadi namba moja ya chama hicho. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Swali limeibuka kwamba, kwanini awe mwanachama namba moja wakati leo ndio amejiunga? Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama hicho ndiye aliyemkabidhi kadi hiyo wakati wa mkutano wa kumkaribisha uliofanyika leo katika Ofisi za Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Kwenye mkutano huo Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho amefafanua kuwa, chama hicho kilianza kikiwa na wanachama wengi na kwamba, kadi za kwanza kwenye chama hicho zilikuwa ‘premium’ (za malipo) hivyo, watu hao kwa sasa hawapo kwenye chama hicho.

Kutokana na kuondoka kwa wanachama hao, kadi hizo zilibaki zikiwa hazina wanachama kwa kipindi chote hicho huku zikibaki kuwa na hadhi ile ile.

“Chama hichi kilikuwa na wanachama ambao sasa hivi hawapo. Ndio waliokuwa wanachama wa chama hiki. Tukasema kadi hizi premium ndizo tutazotumia kwa wanachama hawa,” amesema.

Zitto amesema kuwa, baada ya wanachama waliochukua kadi hizo za awali kuondoka, kazi hizo zimebaki na kutokuwa na mtu yoyote hivyo, kutokana na hadhi yake ‘premium’ ndio maana amepewa Maalim Seif na namba zilizofuata ambazo hazina wanachama kwa sasa wamepewa waandamizi wengine waliotoka CUF na kujiunga na chama hicho.

“Niwaeleze tu Maalim Seif kadi yake ni namba moja (No.1), kuna mwanachama mmoja aliyemnunulia kadi hii na kuilipia kwa miaka 10,” amesema Zitto na kuongeza;

“Kadi hii imelipwa na mwanachama anayeitwa Venance Masebo ambaye alisema, acha mimi niilipie kadi hiyo kwa ajili ya Maalim Seifna ameilipia ada ya miaka 10.”

Kadi za wanachama hao wapya pia zilinunuliwa na watu wengine akiwemo Omar Said Shaaban, Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar aliyenunua kadi namba nne Mansour Yusuf Himid. Huyu aliwahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki (CCM) na baadaye alijiunga na CUF.

Ismail Jusa Ladhu, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF amenunuliwa kadi namba 17 na kadi namba sita akinunuliwa Nasor Mazrui ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar.

Babu Juma Duni Haji amekabidhiwa kadi namba 10 huku Zitto akimnunulia Joran Bashange, aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha CUF kadi namba mbili.

Kadi ya Salim Biman, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma imeelezwa itapelekewa Zanzibar kwa kuwa, amebaki akifanya kazi maalim.

Maalim Seif amekwenda leo kwenye ofisi za ACT-Wazalendo akiongozana na waliokuwa viongozi wa CUF ambao wote kwa pamoja walipewa kadi za chama hicho.

Kwenye mkutano huo Malim Seif amesema, “hatukuja kuteka chama. Tumekuja kuongeza nguvu ili kufikia malengo. Nchi hii inahitaji kurejeshwa kwenye misingi ya kidemokrasia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!