Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kwa mara ya kwanza Dk. Bashiru atema nyongo bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Kwa mara ya kwanza Dk. Bashiru atema nyongo bungeni

Spread the love

 

DAKTARI Bashiru Ally, Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, leo tarehe 25 Mei 2021, amesimama bungeni kwa mara ya kwanza na kutumia jukwaa hilo kuzungumzia masuala mbalimbali yaliyojitokeza nchini, tangu aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, kufariki dunia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, kwa ugonjwa wa moyo, katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, kisha mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi mwaka huu.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, Dk. Bashiru amesema Tanzania ilipitia misukosuko mingi kufuatia kifo cha Magufuli, lakini kwa neema za Mungu, ilivuka salama.

“Kwa kuwa ni mara ya kwanza kuongea, nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutuneemesha na kuivusha nchi yetu, katika kipindi cha misukosuko baada ya kupata msiba mkubwa ambao haujawahi kutokea katika nchi yetu. Ninahakika Mungu hatatutupa,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru Ally

Dk. Bashiru aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi siku za mwisho za uongozi wa Magufuli, amesema baada ya kifo cha kiongozi huyo kutokea, kulitokea majaribio kadhaa yaliyokuwa na lengo la kuitikisa nchi, lakini hayakufanikiwa.

“Yalikuwepo majaribio ya kupitisha maneno na kutuchonganisha, wakati mwingine kudhalilisha watu na kutunga maneno ya uongo, ili nchi itikisike. Lakini nasema wameshindwa na wamelegea,” amesema Dk. Bashiru.

Tarehe 27 Februari mwaka huu, Magufuli alimteua Dk. Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, baada ya aliyekuwa anashika nafasi hiyo, Balozi John Kijazi, kufariki dunia.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo alihudumu kwenye nafasi hiyo kwa muda wa siku 32, baada ya Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan, kumteua kuwa mbunge kisha nafasi hiyo kuikabidhi kwa Balozi Hussein Katanga.

Dk. Bashiru amempongeza Rais Samia, baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Mgufuli, akiwa sambamba na mtoto wa marehemu pamoja na katibu mkuu kiongozi Dk. Bashiru Ally

Aidha, Dk. Bashiru amemshukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa mbunge, huku akimuahidi kutomuangusha katika kuitumikia nafasi hiyo.

“Kwa kuwa mimi ni mbunge wa rais na ni upendeleo mkubwa sababu ziko nafasi 10 tu za kikatiba na hadi sasa tuko wanane. Nimshukuru sana Rais Samia kwa kuniamini na nimuahidi kwamba sitamuangusha,” amesema Dk. Bashiru.

1 Comment

  • Alikufa kwa ugonjwa wa moyo katika hospitali ya Mzena?. Si tuna Kikwete Heart Hospital na waatalamu wake waliobobea kina Profesa Jeneby? Kwanini asilazwe huko?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!