September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kutimuliwa ubunge: Zitto akingiwa kifua

Juma Duni Haji, Naibu Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo

Spread the love

DHAMIRA ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kutaka kumtimua Zitto Kabwe bungeni, kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), imepingwa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Juma Duni Haji, Naibu Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo amesema, Zitto hajazuia mkopo wa elimu kutoka Benki ya Dunia (WB).

Amesema, Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho, ameweka bayana kile kinachowakumba wanafunzi wa like nchini.

Na kwamba, dhamira ya Zitto, Mbunge wa Kigoma Mjini, ni kuitaka serikali ihakikishe uwepo wa mfumo madhubuti wa wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

Duni ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Februari 2020, katika ofisi za chama hicho Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

“Spika Ndugai aliwaongoza wabunge wa CCM kumjadili, kumkejeli na kumdhihaki Zitto Kabwe kwa kitendo chake cha kishujaa cha kuiandikia Benki ya Dunia barua, kuitaka isitishe mkopo kwa serikali hadi itapoweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba kuendelea na masomo.

“Mbunge Abdallah Bulembo alikwenda mbali zaidi na kupendekeza kuwa Zitto Kabwe auwawe, tumejiridhisha bila shaka kulikuwa na nia ovu,” amesema Duni.

Ameeleza kuwa Spika Ndugai amelidhalilisha Bunge kwa kitendo cha kuongoza wabunge hao kumadhihaki Zitto hadi wengine kufikia kiwango cha kumtishia uhai wake na kuwa wao kama chama wanaamini Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amefanya kitendo cha kishujaa na kizalendo.

“Zitto amefanya kitendo cha kizalendo katika kuiwajibisha serikali ambayo kimsingi ndiyo kazi ya Bunge na kuwa lilipaswa kupitisha azimio la kumpongeza kwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo,” amesema Duni.

Ikumbukwe kuwa tarehe 22 Juni mwaka 2017 Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi mkoani Pwani wakati akizundua daraja la Ruvu Chini alinukuliwa akisema ‘Ndani ya utawala wangu kama Rais hakuna mwenye mimba atakaye rudi shuleni, hakuna mtu mwenye mtoto atakayerudi shuleni amechagua maisha ya mtoto akalee vizuri huyo mtoto’.

Kauli hiyo ya Rais ilizua mjadala mkubwa nchini na kupingwa vikali na wanaharakati mbalimbali pamoja na vyama vya siasa wakieleza kuwa ni kinyume na haki za binadamu.

Hata hivyo Duni ameihoji Serikali kuwa kama ilikuwa inataka kupata mkopo huo kutoka Benki ya Dunia imeshindwaje kuzingatia madai ya Zitto? na kwakuwa hoja hujibiwa kwa hoja serikali ina nafasi ya kukutana na Benki ya Dunia na kutoa majibu ya kujiridhisha ili mkopo huo utoke.

Duni amesema Chama hicho kimechukulia kwa uzito suala la vitisho vya wabunge wa CCM dhidi ya Mbunge wao na kuwaeleza kuwa lolote baya litajalomkuta Zitto waliomtishia watawajibika kikamilifu hivyo chama kimewaweka katika hali ya tahadhari wanachama wake nchi nzima kuhakikisha wanamlinda kiongizi huyo.

error: Content is protected !!