January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kusimamisha bomoabomoa ni ‘danganya toto’

Spread the love

WAHANGA wa sakata la bomoabomoa lililoanza wiki iliyopita katika bonde la Mto Msimbazi, Kinondoni Mkwajuni wamesema agizo la kusimamisha zoezi la ubomoaji huo hadi Januari hautasaidia lolote. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Zoezi hilo lililoanza Desemba 17 mwaka huu limesitishwa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5, 2016 kwa kigezo cha kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe na mali zao.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online, wakazi wa maeneo yanayotarajiwa kubomolewa ifikapo Januari wameoneshwa kutoridhishwa na muda uliotolewa kwa kuwapa nafasi za kutoa na kuhamisha makazi yao katika mabonde hayo.

“Ni muda mchache sana wa kufanya maandalizi ya kutoa vitu vyetu kwa sababu hatuna sehemu ya kuvipeleka hata hivyo kupata nyumba kwa hapa mjini ni shida, haiwezekani kupata ndani ya siku sita hizo,” amesema mmoja wa wahanga hao aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna Samson.

Muhanga mwingine, Asha Salum amesema hatua ya kusimamisha zoezi hilo ingefanyika kabla ya kuanza kubomoa hivyo kitendo walichokifanya cha kubomoa kwa kuwakurupusha kisha kuwapa siku sita mbele kwa ajili ya maandalizi wakati tayari baadhi yao wameshaingia hasara ya kubomolewa.

error: Content is protected !!