Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kushambuliwa Mbowe: ‘Issue’ ni Uchaguzi Mkuu
Habari za Siasa

Kushambuliwa Mbowe: ‘Issue’ ni Uchaguzi Mkuu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TAARIFA za awali zinaeleza, shambulizi alilofanyiwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) – Taifa, lina uhusiano na uchaguzi mkuu 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

 “…wakamuambia wewe unaisumbua sana serikali, tunataka tukuoneshe kama serikali ipo, sisi hatuna mpango wa kukuua ila tunataka tukuvunje, ili ushindwe kufanya kampeni,” amesema Mchungaji Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini akinukuu mazungumzo yake na Mbowe leo asubuhi tarehe 9 Juni 2020.

Mbowe alishambuliwa usiku wa manane wa kuamkia leo wakati akirejea katika makazi yake yaliyopo eneo la Area D, jijini Dodoma. Alishambuliwa na watu watatu na wamemvunja mguu. Kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya DCMCT Ntyuka jijini humo.

Akizungumzia mazungumzo yake na Mbowe, Msigwa amesema wakati mwenyekiti huyo akipanda ngazi kwenda nyumbani kwake, walishuka watu watatu wakiwa wamevaa makoti meusi.

“Watu hao ndio walimwambia kwamba anaisumbua sana serikali, na kwamba hawana mpango wa kumuua ila wanamvunja ili ashindwe kwenda kwenye kampeni za uchaguzi mkuu,” amesema Msigwa na kuongeza:

“Tuna amini hii ni shambulio dhidi ya demokrasia kutuzuia tusiseme na uhuru wa kujieleza.  Ni aibu wabunge tunashambuliwa kwa mara ya pili tukiwa katika eneo la Bunge.”

Baada ya kumtembelea Mbowe hospitalini hapo, Eather Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini amesema, kwa sasa wanafanya utaratibu wa kumhamishia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Bulaya ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amewataka wanachama wa Chadema na Watanzania kwa ujumla, kumwombea Mbowe ili apone haraka.

“Mbowe amevunjika mguu wa kulia, tumefanya utaratibu kuhakikisha anakwenda Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Watanzania wawe na subira , waendele kumuombea,” amesema Bulaya.

Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge na Job Ndugai, Spika wa Bunge, wamehudhuria hospitalini hapo kwa ajili ya kumuona Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Akizungumzia hali ya Mbowe, Dk. Tulia amesema, madakatari wanaendelea kumfanyia vipimo kwa ajili ya kuangalia ameumia kwa kiasi gani.

“Kwa sasa hivi siwezi kusema anendeleaje, lakini wanaaendelea kufanya uchunguzi, kikubwa kilichopo sasa hivi ni maumivu ya mguu,”amesema Dk. Tulia.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema amesema, taarifa za kushambuliwa kwa mwenyekiti wa chama chake ‘ni taarifa mbaya kuisikia.’

Amesema, wakati ‘timu ya kusifu’ ikifurahia Uhuru wao, wakiishi maisha yao, viongozi wa upinzani wanaishi kwa woga na wengine kujifungia kama wafungwa kwa sababu ya kupigania utawala bora.

Miaka mitatu iliyopita, Lissu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki alishambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, Area D jijini humo.

Lissu alimiminiwa risasi zaidi ya 30 na 16 kumpata mwilini mchana wa tarehe 7 Septemba 2017, na kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali, na baadaye kusafirishwa kwa ndege hadi Nairobi, nchini Kenya na kisha Ubelgiji alipo mpaka sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!