Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kura za maoni: Chadema Ubungo kwapasuka
Habari za Siasa

Kura za maoni: Chadema Ubungo kwapasuka

Spread the love

KURA za maoni ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Ubungo, zimeacha mpasuko. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Baadhi ya watia nia ndani ya chama hicho, wameamua kuhama huku wengine wakikimbilia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuomba mwongozo.

Mpasuko huo, ulifika tamati baada ya Chadema Kanda ya Pwani tarehe 11 Julai 2020, kuamua kuvunja uongozi wa Chadema Wilaya ya Ubungo.

Taarifa za awali zimeeleza, msuguano ulianza kushika kasi baada ya baadhi ya wajumbe kuonesha nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo.

Viongozi wa Chadema Wilaya ya Ubungo, wameeleza kupinga hatua ya Kanda ya Pwani kuvunja na hatimaye kuwavua nyazifa walizokuwa nazo, wakisema ‘chama kimesigina Katiba yake.’

Renatus Pamba, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilayani humo leo tarehe 14 Julai 2020, ameiambia MwanaHALISI Online kwamba, tangu alipochukua na kurudisha fomu ya kuomba kuteuliwa, yeye na wenzake walianza kuandamwa.

“Kila mwanasiasa ana malengo yake. Mimi nilitia nia kugombea Ubungo, baada ya kuonesha nia, zilizanza figisu za kuvunja Kamati Tendaji ya Jimbo ambayo inatoa mapendekezo ya nani awe mgombea na jina liende Kamati Kuu, lakini ndio kamati inayoratibu shughuli zote,” amesemai.

Pamba amesema, yeye na wenzake ambao hakutaja majina yao, wameomba kujiunga Chama cha ACT-Wazalendo, ili kuendeleza mapambano ya kudai demokrasia.

“Sisi hatukubaliani na maamuzi yale. Tunafanya maamuzi ya kwetu. Leo hii tunaachana na Chadema, tunaomba kujiunga na ACT-Wazalendo.

“Sababu tumeona uchaguzi ndani ya chama hicho (Chadema) kulikuwa na mgombea wao wanayemtaka ashinde,” amesema Pamba.

Amesema, ameitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kufuatilia mienendo ya vyama vya siasa, ili kuhakikisha vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria.

“Wamevunja uongozi Jumamosi, wakatangaza Jumatatu tunarudia uchaguzi, Jumanne wanarudia uchaguzi na watu wanataka watu wachukue fomu na wapate wadhamini hapo hapo,” amesema Pamba na kuongeza “hayo mambo Msajili wa Vyama vya Siasa aangalie.”

Alex Mtamwega, Katibu Mwenezi Chadema Wilaya ya Ubungo amesema, mgogoro huo umetokana na mnyukano wa kinyanganyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwenye jimbo hilo.

Mtamwega amedai, uongozi wa Chadema Jimbo la Ubungo umevunjwa kinyume cha Sheria na Katiba ya Chadema ili kutetea mtu mmoja.

Mtamwega amedai “leo unafanyika uchaguzi mpya wa kuchagua viongozi wapya kitu, ambacho sijawahi kuona unachukua fomu ukumbini, unajaza hapohapo na unachaguliwa. Hatujawahi kuona kitu kama hicho.”

Ashura Kalovya, Mwanachama wa Chadema Kata ya Makurumla akizungumzia sakata hilo amesema, viongizi watakaochaguliwa leo watakuwa batili na si halali.

Kalovya amewataka viongozi wa juu kuliangalia suala hilo, ili lisilete athari katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Uchaguzi wa leo ni batili, sio halali na watakaopitishwa sio halali wa mkutano mkuu wa chama. Kamati Kuu na uongozi wa chama waingilie jambo hili kwa mustakabali wa chama.

“Leo Chadema inapoelekea, inakwenda kuanguka na hata uchaguzi mkuu sidhani chama chetu kitavuka,” amesema Kalovya.

Deogratius Mtoshu, aliyekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema Taifa na Katibu Mwenezi Kata ya Kimara, pia ametangaza kuhamia ACT-Wazalendo.

Hemed Ally, Katibu wa Kanda ya Pwani Chadema alipoulizwa juu ya madai ya wajumbe hao, amejibu “nitatoa ufafanuzi muda mfupi ujao.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!