July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchakato kura za maoni Chadema hadharani

Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya mchakato wa kura ya maoni nafasi ya ubunge wa majimbo na uteuzi ndani ya chama. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Tumaini Makene, Afisa Habari wa chama hicho, inasema 20 -25 Julai mwaka huu, kutafanyika kura ya maoni kwa wabunge wa majimbo na wabunge wa viti maalum kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

“Kanda Pwani inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kura ya maoni itafanyika 20 – 25 Julai mwaka huu huku kanda ya Nyasa inayojumuisha mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Sogwe na Mtwara kura ya maoni ikifanyika 20 – 24 Julai,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, 21 – 25 Julai mchakato huo utafanyika kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi na kanda ya Victoria inayojumyisha mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita.

Pia, mchakato huo utafanyika 20 – 25 Julai katika kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga. Wakati Singida itakuwa ni 21 – 25 Julai. Kwa upande wa kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara mchakato utafanyika 22 – 25 Julai.

error: Content is protected !!