MSIMAMIZI wa uchaguzi kura za maoni jimbo la Mufindi Kusini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sadiki Kadulo amewataka wajumbe na watia nia kufuata utaratibu ili kuepusha vurugu ukumbini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea)
Kadulo amesema hayo leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 wakati akitoa utaratibu jinsi ya wajumbe watakavyopiga kura za maoni kuchagua mgombea wanaye mtaka.
Amesema kura za maoni ni sehemu ya mchakato wa uteuzi, lakini kuteuliwa itategemea na sifa na matendo ya mgombea.
Aidha amesema, mgombea ama mjumbe ambaye hatofuata utaratibu hawatasita kumtoa ukumbini.
“Ni imani yangu mkutano utakuwa huru na haki kwani uchaguzi ni sehemu ya demokrasia,” amesema.
Jimbo la Mufindi Kusini lina wajumbe 612 waliofika katika ukumbi huo ni 604 ambao ndio wajumbe halali wa mkutano huo huku jimbo likiwa na kata 16.
Waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni 31 akiwamo mbunge anayemaliza muda wake, Mendrad Kigola.
Endelea kufuatulia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari mbalimbali
Leave a comment