Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kura za chuki zanukia CCM 
Habari za SiasaTangulizi

Kura za chuki zanukia CCM 

Humphrey Polepole, Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

BAADAHI ya maeneo nchini, wateule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 24 Novemba 2019, wanaweza kukumbwa na kura za chuki. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ni kutokana na baadhi ya wagombea wake kupitishwa huku wakilalamikiwa na wajumbe, kwamba wamebebwa kwa maslahi binafsi.

Malalamiko yamejikita katika kutangaza wagombea walioshindwa, mgombea kulalamikia kutotendewa haki wakati wa kuhesabu kura na hata wagombea walioshindwa kukataa kusaini fomu.

Kata ya Ipagala, Mtaa wa Ilazo Bwawani jijini Dodoma, baadhi ya wanachama wa chama hicho, wameahidi maajabu wakati wa kupiga kura za kumchagua mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo.

Wamesema, wako tayari kumpigia mgombea yeyote wa upinzani kwa madai Musa Thabiti, alipitishwa kwa ‘mizengwe’ sio chaguo lao, pia hakushinda kwenye kura za maoni. Kwa sasa Thabiti ndio anamaliza muda wake kama Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ilazo Bwawani.

Taarifa zaidi zinaeleza, Thabiti alishindwa kwenye kura za maoni, lakini Dotto Gombo, Diwani wa Kata ya Ipagala na marafiki zake wengine, wanataka kuhakikisha anarejea madarakani.

Bakari Dede, mjumbe na mwanachama wa CCM kwenye kata hiyo amedai, Thabiti hakuweza kuunganisha watu na badala yake alikuwa akitengeneza makundi.

Anadai, Albert Nyau ambaye alikuwa Balozi wa CCM Shina No. 4 Ilazo Bwawani, ndiye aliyeshinda kwenye kura za maoni za kugombea nafasi ya uenyekiti wa mtaa huo.

Rehema Waziri, mwanachama na mkazi wa kata ya Ipagala, mtaa wa Ilazo Bwawani amesema, wanachama hao wamefikia hatua ya kuweka maazimio ya kutokuwa tayari kumpigia kura Thabiti.

“Sisi wananchi wa mtaa wa Ilazo Bwawani, zipo kaya zaidi ya 150 na maeneo yetu hayajapimwa, tumeomba sana kushughulikiwa lakini mwenyekiti (Thabiti) anakwepa, mbaya zaidi ni pale ambapo diwani anatuambia yeye (Thabiti) atakuwa mwenyekiti wa mtaa huo hadi kufa,” amesema Rehema na kuongeza;

“Kutokana na hali hiyo, sisi hatupo tayari kumpigia kura mtu ambaye hajawahi kututetea na badala yake anafanya kazi kwa masilahi yake binafsi.”

Naye Thabiti amesema, hajui tuhuma zinazotolewa dhidi yake na wala matokeo hayajabadilishwa “ninachojia zilipigwa kura na zikatosha na kutangazwa kuwa mshindi katika kuraza maoni, hivyo niapeperusha bendera ya chama.”

Anayetuhumiwa kumpigia kampeni, Dotto Gombo ambaye ni Diwani wa Kata ya Ipagala, amekana kuhusika na kumtengenezea ‘dili’ la ushindi Thabiti, “huo ni uzushi tu, mimi siwezi kufanya hivyo.”

Gombo amesema, kura za maoni zilipigwa na kwa baadhi ya wagombea kura zilirudiwa na kufanya kuwepo kwa mchujo wa watu wawili.

Na kwamba, kesho yake walipanga kupiga kura lakini wapenzi wa Albert Nyau, hawakurudi kupiga kura pamoja na mgombea kwa maana nyingine walisusa.

“Wakati wa kupiga kura, upande wa Nyau walisusa, hawakuja na mgombea hakuja lakini kura zilipigwa na matokeo yake Thabiti akaonekana mshindi.

“Sasa hapo unawezaje kusema matokeo yalipinduliwa, watu wasifanye siasa za kuchafuana, walichokifanya wao wanakijua na kama wanasema kuwa watapigia kura upinzani, hapo sijui uzalendo wao ndani ya chama huko wapi?” amehoji Gombo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!