Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kundi la Thelathini kwa Thelathini laanzishwa Kagera
Habari Mchanganyiko

Kundi la Thelathini kwa Thelathini laanzishwa Kagera

Miche ya miti ya Parachichi
Spread the love

 

KIKUNDI cha Thelathini kwa Thelathini/ Gashatu Omu Gashatu wamejipanga kubadili maisha ya wananchi wa Kagera kwa kumwezesha kitaalam kuujua mparachichi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Kundi hilo limethamilia kuhakikisha hadi Oktoba 2022 miche zaidi ya milioni inakuwa imepandwa, kuitunza, kukuza na kuvuna miparachichi yenye viwango vinavyokubalika soko la dunia.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kundi hilo, Wilfred Rwakatale alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online kuhusu mpango huo ambao utazinduliwa Aprili 2022.

Amesema kesho tarehe 17 Machi 2022 wataendesha mafunzo mjini Bukoba kwa watu mbalimbali watakaojitokeza kuhusu umuhimu wa upandaji miche ya maparachichi ambayo ni dhahabu juu ya ardhi.

Rwakatale aliyewahi kuwa mbunge wa Bukoba Mjini amesema, mafunzo na mjadala yataendeshwa na wataalam waliobobea kwenye kilimo Cha kibiashara cha zao la Parachichi HASS.

Amesema hadi kufikia Oktoba 2022 wanataka miche zaidi ya milioni moja iwe imepandwa “tumejiwekea malengo yanayotekelezeka.”

Aidha, wadau watapata fursa ya kuwafahamu waratibu wakuu wa mradi huu wa Thelathini kwa Thelathini kwq kupata uzoefu wao na mbinu za kufanikisha katika kilimo hicho.

Rwakatale amesema, mafunzo hayo yataanza saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku, katika ukumbi wa LWAX B&B COMFORT ARENA Kibeta Kankwilwa.

Amesema wanaotaka kushiriki mafunzo hayo wanapaswa kujisajili kupitia simu namba 0767433818/ 0716768844/ 0756521126 na kulipia ada ya mafunzo Sh.25000 kwa ajili ya chakula, kinywaji cha kutosha bila kukosa burudani mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!