Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Tangulizi Kundi la 17 lenye wananchi 179 lahama Ngorongoro
Tangulizi

Kundi la 17 lenye wananchi 179 lahama Ngorongoro

Spread the love

 

KUNDI la 17 la wananchi wanaohama kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine limeondoka leo tarehe 12 Januari, 2023 baada ya kuagwa na Viongozi wa Mkoa wa Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa Naibu Kamishna wa Uhifadhi NCAA, Dk. Christopher Timbuka, kundi linalohama katika awamu hii linajumuisha kaya 34 zenye wananchi 179 pamoja na Mifugo 625.

Ameongeza kuwa kati ya Kaya 34 zinazohama katika awamu hii, kaya 30 zinahamia Kijiji cha Msomera Mkoani Tanga na kaya 4 zinahamia maeneo mengine ya nchi waliyochagua kwa hiari yao.

Naibu Kamishna Dk. Timbuka ameeleza kuwa zoezi la kuhamisha wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera lililoanza mwenzi Juni, 2022, hadi kufikia tarehe 12 Januari, 2023 Jumla ya kaya 523 zenye watu 2,808 na mifugo 14,757 zimeshahamia Kijiji cha Msomera na maeneo mengine kwa ajili ya kupisha shughuli za Uhifadhi katika eneo la Ngorongoro.

Akiwaaga wananchi hao Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwalla amesema zoezi la kuwaandikisha wananchi wanaotaka kuhama kwa hiari ndani ya hifadhi hiyo inaendelea na Serikali inawapa stahiki zao ikiwa ni pamoja na kuwapa fidia inayostahili pamoja na kuwasafirishia mizigo na mali zao kuelekea kwenye makazi mapya.

“Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imewapa wananchi uhuru wa kuhama kwa hiari, kila mwananchi aliyeko tayari kuhama anafanyiwa tathmini ya mali zake na kupewa fidia pamoja na kuwezeshwa usafiri yeye na mali zake ikiwemo mifugo kwenda eneo alipochagua” ameongeza Mangwala.

Mangwala ameongeza kuwa kadri wananchi wanavyoondoka katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro imeongeza utulivu wa hifadhi na Wanyama hali iliyoongeza hamasa ya utalii hasa kipindi cha mwisho wa mwaka 2022 na mwanzo wa mwaka 2023 ambapo kwa mwezi Desemba, 2022 pekee watalii takribani 63,248 wametembelea vivutio vilivyoko eneo la hifadhi ya Ngorongoro.

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Masaile Mussa amewaeleza wananchi wa Ngorongoro kuwa Serikali ya mkoa huo itaendelea kuwahakikishia usalama wananchi wote wanaojiandikisha kuhama kwa hiari na misingi yote ya utu na haki za binadamu itazingatiwa.

Lapajara Tauwo ambaye ni miongoni mwa wananchi wanaohama ameeleza kuwa

“Mwanzo nilikuwa nasita kuhama lakini baada ya kuwasiliana na wenzangu waliohamia Kijiji cha Msomera nimeona na mimi niondoke nikawe huru kufanya shughuli za uzalishaji mali na ujasiriamali, naamini hata ndugu zetu tuliowaacha Ngorongoro watahamasika na kujiandikisha kwa wingi zaidi ili tuache hifadhi yetu ilete faida kwa maslahi ya watanzania wote,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!