August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kumekucha uchaguzi mdogo Sengerema.

Ander Herrera

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Sengerema kimeanza kampeni zake kwa kasi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kahumulo, na kuwataka wananchi wasimchague mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika tarehe 22 Januari 2017, anaandika Moses Mseti.

Katika mkutano huo wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho uliofanyika kijiji cha Nyitundu Emmanuel Munwanis, diwani wa kata ya Nyumpulukano (Chadema) amesema;

“Wananchi wa Sengerema mnapaswa kufahamu kwamba Chadema ni chama makini ambacho kina malengo ya kuwaletea maendeleo, hivyo wakazi wa kata hiyo mnapaswa kumuamini mgombea wa chama hiki kwani ndiye anafaa na anajua matatizo ya kata yenu na njia za utatuzi wake,” amesema.

Munwanis ambaye ndiye meneja wa kampeni za Chadema katika kata hiyo, amesema lazima wananchi waelewe na kukubali mabadiliko katika nchi hii, na kwamba uchaguzi mdogo wa kata hiyo uwe mwanga wa mabadiliko ya maendeleo ya kata hiyo na uwe mwanzo wa wananchi wanyonge kutetewa kwa vitendo.

John Dotto, Mgombea wa chama hicho, amewaomba wananchi kumchagua kwa kura nyingi ili aweze kuwa diwani wa kata ya Kahumulo huku akiahidi kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo.

“Haiwezekani wananchi wakaendelea kunywa maji kutoka kwenye madimbwi sawa na mifugo na hatiamaye kuishia kuugua na kutumia gharama kubwa kutibu magonjwa wanayougua kwa kunywa maji machafu,” amesema.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Nyitundu aliyehudhuria  uzinduzi wa kampeni hizo, Juma Kayanda, ameiambia MwanaHALISI Online kuwa, “vyama vya siasa vinatakiwa kutoa sera za kuwasaidia wananchi na kwamba yeye ameguswa sana na sera za Chadema huku akiwataka wenzake wasikilize sera za wagombea wote ili mwisho wa siku wawe na uamuzi sahihi badala ya kuchagua kwa ushabiki.”

Uchaguzi wa Kata ya Kahumulo umekuja baada Joseph Kando, maarufu “Njiwa pori” aliyekuwa diwani wa kata hiyo (CCM) kujiuzulu wadhifa huo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa chama chake.

 

error: Content is protected !!