August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Kulima kisasa kunafungua masoko’

Spread the love

WAKULIMA nchini wametakiwa kulima kisasa zao la mahindi na kuhifadhi vizuri kulingana na vigezo vinavyostahili ili kuweza kupata soko la ndani na nje ya nchi, anaandika Christina Haule.

Emmanuel Msuya, Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Dar es Salaam (Kipawa) amesema hayo kwenye Maonesho ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Mashariki (TASO) yanayofanyika katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Morogoro.

Msuya amesema, wao kama wakala hununua mazao yaliyolimwa kwa kuzingatia vigezo vyenye ubora huku yakifuata utaalamu unaostahili na kuyagawa pindi panapotokea majanga ya njaa ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo amesema kuwa, pia huuza mazao hayo ndani na nje ya nchi ikiwa maghala yao yatakuwa yamejaa vyakula.

Amesema, katika msimu huu wanaanza kununua mazao mkoani Morogoro kwenye kituo chao kilichopo Masika ambapo amewaagiza wakulima kujitokeza kuuza mazao yao kufuatia wao kununua kwa bei ya Sh. 5000 kwa tani moja.

Aidha, amefafanua kwamba, kufuatia kuwa wakala wa Taifa, huuza mazao hayo kwa jamii inayokumbwa na majanga ya njaa, mafuriko na mengineyo kwa bei nafuu hadi Sh. 50 kwa kilo moja.

Hivyo amesema, wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mahindi ya kutosha kutokana na hali mbaya ya uzalishaji ambapo mwaka 2015 walifanikiwa kununua tani 22 za mahindi na kuyahifadhi kwenye maghala yao na kwamba, mwaka 2020 wanatarajia kununua tani laki nne na kuzihifadhi kwenye maghala.

error: Content is protected !!