January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kujua bei, makato ya mikopo ya nyumba sasa mtandaoni

Ramani ya Mradi wa DEGE Kigamboni

Spread the love

KAMPUNI ya Lamudi Tanzania imeanzisha programu maalum ya kikokotoleo cha mikopo nyumba, ambacho kitamwezesha mteja kujua kiasi cha kulipa na muda atakaolipa kupitia kwenye mtandao wa kampuni hiyo. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Programu hiyo itamwezesha mteja kujua bei ya nyumba, kiasi atakachokatwa na muda atakaolipa, kupitia miradi mikubwa kama DEGE, COMFORTZONE, LOWMUS, GALAXY ESTATE, MAKAZI SOLUTION na HORN AFRICA.

Meneja wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa ameliambia MwanaHALISI Online, kuwa kikokotoleo hicho kinapatikana kenye mtandao wa Lamudi Tanzania ambao utampa mnunuzi bei pamoja na kiasi atakachokatwa kwa muda anaoutaka.

Nyagawa anasema: “Wanunuzi wa nyumba wanatakiwwa kwenda moja kwa moja kwenye mtandao wa Lamudi na kuchagua nyumba wanayotaka kununua kutoka katika miradi hiyo mikubwa na watapata fulsa na kujua bei na makato watakayokatwa. Mfano mteja akitaka kukatwa kwa miaka 30 ataoneshwa kiasi atakachokatwa kwa mwezi.”

Meneja huyo anasema kikokotoleo hicho kinaonekana kwenye mtandao wa Lamudi upande wa kulia, ambapo ukiingia mteja atakuwa mirado yopte mikubwa na kumpa fulsa ya kuchagua aina ya nyumba na kupata bei zake.

Naye Mkurugenzi wa Lamudi Tanzania, Mustafa Suleimanji, anaongezea: “Timu yetu kwa sasa inaendelea na mazungumzo na benki mbalimbali za Tanzania. Tayari CRDB tumekubaliana nayo kushirikiana nasi kwenye kikokotoleo hicho na tutaendelea na ushirikiano na benki nyingine.”

error: Content is protected !!