May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kuiona Yanga vs Pyramids FC Sh. 10,000/=

Frederick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga

Spread the love

KLABU ya Yanga leo imetangaza rasmi kiingilio kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza, ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 10,000 na cha juu Sh. 70,000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea).

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela amesema kuwa sababu ya kuweka kiingilio hicho ni kutokana na udogo wa kiwanja ambacho kinaingiza mashabiki wachache ukilinganisha na uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Tumeweka kiingilio cha Sh. 10,000 kwa sababu mapato yatakayopatikana yatakuwa na mgao mkubwa ambapo baadhi ya asilimia zitakwenda TFF, CAF, TRA na gharama za mchezo na ukizingatia uwanja ni mdogo na hivyo Yanga inaweza kukosa mapato,” alisema Mwakalebela.

Aidha kiongozi huyo aliongezea kuwa timu itaondoka kesho kuelekea Mwanza ambapo tarehe 22 itacheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC na siku nne baadaye watacheza mchezo wao dhidi ya Pyramids kwenye uwanja huo huo.

Yanga itawakosa nyota wake watano kuelekea mchezo huo ambao ni Mohammed Issa na Issa Bigirimana wote hawa ni majeruhi, huku David Molinga na Mustapha Suleiman watakaa nje kutokana na kukosa vibali na beki kisiki Lamine Moro atakuwa anatumikia kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Zesco FC.

error: Content is protected !!