July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kuiona Twiga Stars 2,000 Chamanzi

Spread the love

KIINGILIO cha chini cha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Taifa Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake Zimbambwe kitakua Sh. 2,000, anaandika Regina Mkonde.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Machi 4, 2016 katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, mbali na kiingilio hicho cha chini, lakini jukwaa kuu itakuwa Sh. 3,000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Baraka Kizuguto, Afisa Habari wa TFF amesema lengo la kuweka kima cha chini cha kiingilio ni kuwapa fursa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa hamasa wachezaji wa Twiga Stars.

“Mchezo huo ni muhimu sana kwa Twiga na Watanzania kwa ujumla, hivyo wanatakiwa kupewa sapoti kubwa na mashabiki,” amesema Kizuguto.

Twiga Stars ina kibarua kigumu cha kuhakikisha inafuzu kushiriki katika michuano ya Kombe la Afrika kwa wanawake ambapo inabidi ishinde katika mechi hiyo na ile ya marudiano itakayofanyika Machi 18, nchini Zimbabwe.

Anastazia Wambura, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo imetoa kiasi cha Sh. 15 milioni kama motisha kwa wachezaji endapo watafanikiwa kushinda mechi zote mbili.

Wambura amesema, kila mchezaji atapata shilingi 300,000 kwa kila mechi watakayoshinda, na kwamba kama watashinda mechi zote mbili, kila mchezaji atapata Sh. 600,000.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia, huku Kamisaa wa mchezo akitokea nchini DRC Congo.

error: Content is protected !!