December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kuiona Taifa Stars kama Simba

Kikosi cha Taifa Stars wakiwa mazoezini nchini Misri

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Burundi ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Tsh 3,000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa 11 Oktoba 2020 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Kiingilio hiko cha Tsh. 3,000 kimekuwa rafiki kwa siku za hivi karibuni kwa mashabiki mashabiki wa klabu ya Simba ambapo wanatumia kuingilia uwanjani katika michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mechi zao za nyumbani.

Vingilio vingine kwenye mchezo huo vitakuwa Tsh 20,000 kwa VIP A na Tsh 10,000 kwa upande wa VIP B, huku kocha mkuu wa Stars Etiene Ndailagije akitarajia kutangaza kikosi chake 2 Oktoba 2020.

error: Content is protected !!