Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Kuidhikahi picha ya Rais’ kwaendelea kumsotesha Idris Sultan
Habari za SiasaMichezo

‘Kuidhikahi picha ya Rais’ kwaendelea kumsotesha Idris Sultan

Idris Sultani, Msanii wa Vichekesho nchini Tanzania
Spread the love

IDRIS Sultani, Msanii wa Vichekesho nchini Tanzania, leo Ijumaa tarehe 22 Mei 2020, anaweza kufikishwa mahakamani, kwa kosa la kuidhihaki picha ya Rais John Magufuli. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Idris anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo cha Polisi cha Oysterbay,  jijini Dar es Salaam, tangu Jumanne tarehe 19 Mei 2020,  kwa kosa la uonevu kwa njia ya mtandao, ambapo anadaiwa kuicheka picha ya zamani ya Rais Magufuli.

Idris amekumbwa na tuhuma hizo, baada ya video inayomuonesha akiicheka picha ya zamani ya Rais Magufuli, kusambaa mitandaoni.

Benedict Ishabakaki, Wakili wa Idris, akizungumza na Mwanahalisi Online kwa njia ya simu, kuhusu maendeleo ya sakata hilo, amesema Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni, jana liliahidi kumpa dhamana msanii huyo, au kumfikisha mahakamani.

Wakili Ishabakaki amesema Idris alitakiwa kuachiwa kwa dhamana jana, lakini ilishindikana baada ya polisi kueleza kwamba, kuna vitu wanamalizia kuchunguza kuhusu msanii huyo.

“Jana, walimaliza mahojiano naye lakini walitunyima dhamana wakisema kuna vitu wanamalizia kuchunguza, kwa hiyo waliahidi dhamana leo itatoka, au watampeleka mahakamani,” amesema Wakili Ishabakaki.

Wakati huo huo, Wakili Ishabakaki amesema polisi wa Kituo cha Oysterbay wamesema, suala la Idris, linatakiwa kushughulikiwa na makao makuu ya Jeshi la Polisi, ambapo anatakiwa kufikishwa katika ofisi hizo, leo saa tano asubuhi.

“Dhamana inaweza kutoka au watampandisha mahakamani, kwa hali ya jana ni kwamba hili suala ni la makao makuu ya polisi. Kwa hiyo wanamchukua Oysterbay, wanampeleka makao makuu ya polisi. Saa tano asubuhi anatakiwa awe makao makuu ya polisi,” amesema Wakili Ishabakaki.

Hii ni mara ya pili kwa Idris kuingia matatani kwa tuhuma za kuidhihaki picha ya Rais Magufuli, ambapo mwezi Novemba mwaka jana, alikamatwa kwa kosa la kuitumia vibaya picha ya kiongozi huyo wa nchi.

Idris aliihariri picha ya Rais Magufuli kwa kuiweka sehemu ya kichwa chake katika mwili wake, kisha kuchukua picha yake na kuiweka katika kiti cha rais, na kuandika maelezo yenye maudhui ya kutaka kubadilishana majukumu na Rais Magufuli, ili kiongozi huyo apumzike kwa muda.

Lakini sakata hilo lilimalizika baada ya Idris kumuomba radhi Rais Magufuli, mbele ya umma, akisema kwamba dhamira yake haikuwa kumdhalilisha, bali ni kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Michezo

Kusanya maokoto na mechi za UEFA leo

Spread the love  LIGI ya mabingwa barani Ulaya inaendelea hii leo kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

error: Content is protected !!