August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Kuichungulia’ Ikulu ya Dar sasa ruksa

Spread the love

SERIKALI imefuta rasmi zuio la kuwataka watu walio jirani na Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam kutojenga majengo yenye urefu unaozidi ghorofa mbili, anaandika Pendo Omary.

Hapo awali, Serikali ilikuwa imetangaza marufuku hiyo kutokana na sababu zilizotajwa kuwa ni kulinda usalama wa Ikulu, ambako ndipo ofisi na makazi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yalipo.

Akizungumza na wadau wa mipango miji leo jijini Dar es Salaam William Lukuvi, Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema amri hiyo imefutwa kufuatia serikali kuwa mbioni kuhamia Dodoma na kwamba upo mpango mpya wa kuifanya Dar kuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.

“Tumejipanga kulifanya jiji la Dar kuwa kituo halisi cha biashara baada ya serikali kutangaza kuhamisha makao yake Dodoma na tayari tumeanza kuandaa ramani mpya ya jiji la Dar es salam ambapo upimaji unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu,” amesema.

Lukuvi pia amesema maeneo yaliyo na ofisi za serikali ambayo baadhi yake yatageuzwa kuwa ya kibiashara na marekebisho hayo yatakwenda sambamba na udhibiti wa msongamano wa magari hapa jijini.

error: Content is protected !!