December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kugombea urais: Maalim Seif atua mzigo Z’bar

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

KITENDAWILI kwamba Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo atagombea urais visiwani Zanzibar, amekitegua leo. Anaripoti Faki Sosi, Zanzibar…(endelea).

Amesema, kutokana na imani ya Wazanzibari waliyoionesha katika miaka yote aliyogombea urais wisiwani humo, ameamua kurejea ulingoni kupambana na yeyote atakayepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

“…kadri ya siku zinavyozidi kukaribia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na watu mbalimbali wenye shauku ya kutaka kujua kama nitagombea au sintogombea.

“Muda wote huo nimekuwa nikiwaeleza kuwa bado sikuwa nimefanya maamuzi kuhusu jambo hilo, nilihitaji kwanza kufanya tafakuri ya kina pia kupata ushauri kutoka kwa viongozi wenzangu, familia yangu na wazee wa busara ninaowaheshimu. Baada ya kufanya tafakuri hiyo ya kina, nina furaha kubwa leo kuwaambia wananchi wa Zanzibar kwamba kwa sasa nimeishafanya maamuzi.

“…na maamuzi yangu ni kwamba…., kwamba…. kwamba…In Shaa Allah, nitagombea nafasi ya urasi wa Zanzibar kwa mara nyingine tena katika chaguzi mkuu wa mwaka huu 2020,” amesema Maalim Seif.

Akizungumza mbele ya wanahabari visiwani humo leo tarehe 28 Juni 202, Maalim Seif ambaye alijiunga na chama hicho akitokea CUF Machi mwaka huu kutokana na mgogoro wake na Prof. Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti CUF), ametaja sababu tano zinazomsukuma kugombea urais kwa mara ya tano mfululizo.

Kwanza; amesema, hata kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, yeye na wenzake hawakuridhishwa na namna visiwa hivyo (Unguja na Pemba) vilivyokuwa vikiendeshwa.

“Mimi na wenzangu kadhaa tulikuwa haturidhishwi na jinsi nchi yetu inavyoendeshwa. Kwa pamoja tulianzisha vuguvugu au movement ya kuweka shinikizo kwa dola kuruhusi mfumo wa vyama vingi,” amesema.

Pili; Maalim Seif amesema, mwaka 1992 walizanisha Chama cha Wananchi (CUF), kwa malengo ya wazi ya kurejesha haki za Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla ambazo mpaka sasa hazijarejeshwa.

“…lakini serikali ikaamua kutumia dola na taasisi zake na hasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na mahakama, kuingilia chama kile na kukidhoofisha kwa kukikabidhi kwa vibaraka wao ambao walipewa kazi ya kutufukuza uanachama mimi na wenzangu.

Tatu: amesema, amekuwa akiaminiwa kwa kiwango kikubwa na Wazanzibar katika kila chaguzi alipogombea, hivyo si vyema kupuuza imani hiyo.

“Viongozi na wanachama wenzangu waliniamini na kunipa bendera ya chama cha awali mwaka 1995, 2000, 2005 na 2015. Katika chaguzi zote hizo, Wazanzibar walinipa imani zao, na kila uchaguzi kura ziliongezeka.

“Nimeona si uungwana hata kidogo kudharu imani hiyo isiyokwisha kwangu, na amabayo imekuwa ikiongezeka kadiri siku zinavyokwenda, na badala yake ninapaswa kuihshimu,” amesema.

Nne: amesema kwamba, nguvu za giza za watawala zilitumika kupunguza nguvu ya wananchi, pia kulazimisha wagombea wa CCM kutangawa washindi licha ya kukataliwa na Wazanzibari.

“Nimeona kuwa, wakati umefika kwa nguvu hizo za giza za watawala kutambua kuwa, nguvu ya umma inapoamua kamwe haiwezi kushindwa, na kwamba uchaguzi huu tutaulinda ushindi wetu katika hali yoyote ile,” amesema.[checklist][/checklist]

Tano: Maalim Seifa amesema, uchaguzi mkuu 2015, ilikuwa ni tokeo la kubadilisha historia Zanzibar kwa maana Wazanzibari wengi walikataa kuongozwa na CCM.

“…lakini serikali haikujali kwa CCM kwamba imeishapoteza imani kwa Wazanzibar, ilimtumia Jecha (Salim Jecha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar) kupindua matokeo.

“Nimeamua kutaka kuwapa kile walichokitaka mwaka 2015, wadhihirishe tena chaguo lao la mwaka 2015 na kuionesha dunia kuwa, maamuzi ya wananchi ni yale yale,” amesema.

error: Content is protected !!