December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Safari ya Prof. Lipumba kuwa waziri yaiva

Spread the love

PROF. Ibrahim Lipumba, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ameachiwa huru na mahakama ya Hakim Mkazi, jijini Dar es Salaam. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DPP), imewasilisha hati maalum mahakamani hapo kueleza kutokuwa na dhamira ya kuendelea na mashitaka yanayomuhusu Prof. Lipumba na wenzake.

Prof. Lipumba ameachiwa huru siku tatu baada ya kukutana na John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. Prof. Lipumba alikutana na Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Novemba.

Mara baada ya kuwasilisha hati hiyo mahamani, Cyprian Mkeha, hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, ameamuru kufutwa kwa kesi hiyo na kuamuru kumwachia huru.

Prof. Lipumba alikuwa akitetewa mahakamani na Peter Kibatala. Wakili huyo alieleza mahakama kutokuwa na pingamizi na hatua hiyo.

Prof. Lipumba na wafuasi 30 wa chama hicho walishitakiwa kwa madai ya mkusanyiko usio halali, tarehe 22 na 27 Januari mwaka huu, wilayani Temeke.

Mkusanyiko huo ulikuwa maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya mauaji wa 15 waliouawa Unguja na Pemba, Januari 26 na 27 mwaka 2001.

Mongoni mwa wafuasi hao, ni pamoja na Shabani Ngurangwa (56), Shabani Tano au Kasakwa (29), Shabani Polomo (40), Juma Mattar (54), Mohammed Kirungi (40), Athumani Ngumwai (40), Shaweji Mohamed Mketo (39) na Abdul Juma Kambaya (40).

https://www.youtube.com/watch?v=MTgGl5OkGZA

Hata hivyo, tarehe 26 Februari mwaka huu wafuasi hao 30 wa CUF waliokuwa wakikabilia na kesi hiyo, walifutiwa mashitaka na DPP.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Garson Msigwa, Prof. Lipumba alikutana na Magufuli kwa lengo la kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa rais.

Hata hivyo, taarifa za ndani zinadai kuwa, kuachiwa huru kwa Prof. Lipumba, kunachagizwa na kikao chake na Rais Magufuli kabla ya kuunda baraza lake la mawaziri.

Taarifa kutoka Ikulu na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinaeleza kwamba kuna uwezekano mkubwa Prof. Lipumba akateuliwa kuwa mmoja wa mawaziri wa serikali itakayoundwa.

Hata hivyo, taarifa za Prof. Lipumba kuingia kwenye serikali ya Rais Magufuli, zilisambaa muda mchache baada ya kiongozi huyo kujiuzulu uenyekiti CUF sambamba na uenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), tarehe 6 Agosti mwaka huu.

Taarifa hiyo ilidai kuwa kumekuwapo makubaliano kati ya Pro. Lipumba na Magufuli na kwamba, “…atapatiwa nafasi ya uwaziri kwenye serikali yake.”

error: Content is protected !!