April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kufungiwa akaunti: THRDC wampa neno Rais Samia

Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, iwape nafasi ya watu kujitetea, mashirikia na taasisi zinazokabiliana na tuhuma mbalimbali, ili kutoumiza watu wasio na hatia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu tarehe 29 Machi 2021, na Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, wakati anazungumzia sakata la kufungwa kwa akaunti za benki za mtandao huo.

Sakata hilo liliibuka Agosti 2020, ambapo Serikali ya Tanzania, ilifunga akaunti za benki za THRDC kwa muda usiojuliakana, ikiutuhunu mtandao huo kukiuka sheria ikiwemo kushindwa kuwasilisha mikataba ya ufadhili wa wahisani.

Olengurumwa amemshauri Rais Samia kujiridhisha kwanza na taarifa anazopewa kama zina ukweli, kabla ya kuzifanyia maamuzi.

Onesmo Olengurumwa,Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu

“Tujitahidi sana kufanya maamuzi kwa uangalifu sana kwa kujiridhisha kwa mtu yoyote yule au tasisi yoyote ili kuepuka kufanyia kazi taarifa nyingine ambazo si za kweli, baadaye tukajikuta tumeumiza watu bila kuwapa nafasi ya kuwasilkiliza,” ameshauri Olengurumwa.

Akikazia ushauri wake huo, Olengurumwa ametolea mfano hatua ya Rais Samia kumsimamisha kazi badala ya kumfukuza kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdetius Kakoko, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubahirifu wa fedha zilizoibuka katika mamlaka hiyo.

Mratibu huyo wa THRDC amesema, hatua hiyo ya Rais Samia itampa nafasi Mhandisi Kakoko kujitetea kwa mujibu wa sheria.

“Na jana tumeona rais akimsimamisha mtu baadala ya kumfukuza, hii inatoa nafasi ya kusikilizwa na kufanya usawa wakati wa kufanya maamuzi bila kumuumiza mtu na kufuata taatibu za kisheria,” amesema Olengurumwa.

Kuhusu sakata la kufungwa kwa akaunti za THRDC, Olengurumwa amesema, mtandao huo unaendelea kuzungumza na Serikali, na kwamba wakati wowote akaunti hizo zitafunguliwa.

“Suala letu la akaunti tunaendelea kujadiliana na serikali, majadiliano yanaendelea na muda si mrefu suala letu linaweza likaisha sababu tumeshafanya mazungumzo ya ndani na viongozi wa serikali tukijaribu kuelezea na kuwafafanuliwa mambo ambayo walikuwa na wasiwasi nayo. Tunaendelea vizuri muda wowote akaunti zetu zinaweza kuinguliwa,” amesema Olengurumwa.

Akizungumzia athari ambazo THRDC imepata kufuatia hatua hiyo, Olengurumwa amesema, mtandao huo ulishindwa kutekeleza majukumu yake katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2020, ikiwemo kutoa elimu ya mpiga kura na uangalizi wa ndani wa uchaguzi huo. Kutokana na kukosa fedha.

Pia, baadhi ya wafanyakazi wa THRDC wamekosa ajira kutokana na kadhia hiyo.

error: Content is protected !!